Unknown Unknown Author
Title: SHEREHE GEMU 1,000 YAGEUKA MAJANGA ARSENAL, YABAMIZWA 6-0!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SHEREHE na kumbukumbu za Arsene Wenger za kutimiza Gemu 1,000 akiwa Meneja wa Arsenal leo zimekuwa majanga makubwa baada ya Timu yake kutand...

clip_image001[10]SHEREHE na kumbukumbu za Arsene Wenger za kutimiza Gemu 1,000 akiwa Meneja wa Arsenal leo zimekuwa majanga makubwa baada ya Timu yake kutandikwa Bao 6-0 huko Stamford Bridge toka kwa Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, na pia kucheza muda mwingi wa Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada Kieran Gibbs kupewa Kadi Nyekundu, ambayo kama ilistahili, basi aliepaswa kupewa ni Oxlade-Chamberlain na si yeye.clip_image001Ndani ya Dakika 17, Arsenal walikuwa nyuma kwa Bao 3-0 zilizofungwa na Samuel Eto'o, Dakika ya 5, Andre Schürrle, Dakika ya 7 na Penati ya EdenHazard, Dakika ya  17.clip_image001[8]Penati hiyo ya Eden Hazard ilitolewa na Refa Andre Marriner baada Alex Oxlade-Chamberlain kuokoa Mpira kwa mkono lakini Refa huyo alifanya makosa na kumpa Kadi Nyekundu Kieran Gibbs licha ya Oxlade-Chamberlain kumwambia Refa ni yeye alieshika.

Bao nyingine za Chelsea zilifungwa na Oscar, Bao 2, na Mohamed Salah.clip_image001[12]Huu ni ushindi mkubwa kwa Jose Mourinho katika Ligi Kuu England na ni mara ya kwanza kwa Chelsea kuifunga Arsenal Bao 6.

Pia ni Jose Mourinho ambae aliifunga Arsenal wakati Arsene Wenger anatimiza Gemu yake ya 500 na sasa Mourinho hajafungwa na Wenger katika Gemu zote 11 walizokutana.

VIKOSI:CHELSEA: Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, David Luiz; Schurrle, Oscar, Hazard; Eto'o

Akiba: Lampard, Torres, Mikel, Salah, Ba, Schwarzer, Kalas

ARSENAL: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Rosicky, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Podolski, Giroud

Akiba: Vermaelen, Flamini, Fabianski, Sanogo, Jenkinson, Källström, Gnabry

Refa: Andre Marriner

MATOKEO YA MECHI ZINAZOENDELEA KUCHEZWA HIVI SASA:

Live 75' Cardiff City 2 - 5 Liverpool
Live 75' Everton 3 - 1 Swansea City
Live 75' Hull City 2 - 0 West Bromwich Albion
Live 75' Manchester City 3 - 0 Fulham
Live 73' Newcastle United 0 - 0 Crystal Palace
Live 73' Norwich City 2 - 0 Sunderland

MSIMAMO:

NA

TIMU

P

GD

PTS

1

Chelsea

31

39

69

2

Liverpool

29

41

62

3

Arsenal

30

19

62

4

Man City

27

44

60

5

Tottenham

30

-1

53

6

Everton

28

12

51

7

Man Utd

29

12

48

8

Southampton

30

6

45

9

Newcastle

29

-3

43

10

Aston Villa

29

-6

34

11

Stoke

30

-12

34

12

West Ham

29

-6

31

13

Hull

29

-7

30

14

Swansea

29

-5

29

15

Norwich

30

-24

29

16

West Brom

29

-10

28

17

Crystal Palace

29

-19

28

18

Sunderland

27

-16

25

19

Cardiff

30

-29

25

20

Fulham

30

-35

24

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top