Mkuu wa wilaya ya Lindi,Dr Nassor Ally Hamid akifungua mafunzo kwa wanahabari na waratibu wa NHIF/CHF wa mkoa wa Lindi, Kushoto ni Meneja Nhif Lindi, Bi Fortunata Kullaya na kutoka kulia ni Bw Faustine Nzota, Mshauri wa Mfuko wa Afya na anaefuata ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Wilaya ya Nachingwea, Christopher Lilai
Meneja wa NHIF Mkoa wa Lindi akitoa taarifa fupi kuhusiana na mfuko huo katika mafunzo ya wanahabari na waratibu wa Mifuko ya CHF na NHIF Lindi
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali mkoani Lindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Kutoka kulia waliokaa ni Dr Alfred Mukome, Mratibu wa CHF mkoa wa Lindi, Mkuu
wa Wilaya ya Lindi,Dr Nassor Hamid na Meneja wa NHIF Lindi Bi
Fortunata Kullaya
Mratibu wa CHF wilaya ya Liwale akichangia kuboresha mfuko huo katika mkutano wa mafunzo kwa wanahabari na waratibu
Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii mkoa wa Lindi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya
Waratibu wa NHIF mkoa wa Lindi wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa wilaya
Wanahabari na waratibu wa NHIF na CHF wakisikiliza Hotuba ya Ufunguzi toka
Na Abdulaziz Video, LINDI
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja na Mfuko wa Afya ya jamii (CHF) mkoani Lindi, imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa Habari na waratibu wa Mifuko hiyo, ili kuboresha utendaji kazi ili
kutatua changamoto za Afya kwa jamii ya wakazi wa mkoa huo.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo, Meneja wa (NHIF) mkoani hapa, Fortunata Raymond Kullaya ameeleza kuwa mafunzo hayo yaliyojumuisha waandishi wa habari na waratibu kutoka Halmashauri zote sita za mkoa huo yamelenga katika kuboresha utendaji wa kazi na kubaini changamoto mbalimbali zinazokwamisha jamii kujiunga na mifuko hiyo ukiwemo wa Afya ya Jamii(CHF).
Aidha alibainisha kuwa wanahabari wanashiriki vizuri katika
kuhamasisha na kuwapa wananchi taarifa muhimu, zikiwemo za kujiunga na Mifuko hiyo ya (NHIF na CHF) ili kuwaondolea usumbufu pale wanapokwenda kupata huduma za matatibabu pale wanapougua.
Kullaya pia alisema kuwa Ofisi yake imeona upo umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo ili wanahabari waweze kuielimisha jamii iweze kubaini fursa zitakazowezesha utatuzi wa Changamoto hasi na chanya za huduma sanjari na kubadilishana uwezo wa kiutendaji baina yao na watumishi wa mifuko hiyo.
Kullaya akataja sababu nyingine ni pamoja na kuwapa elimu ya
mabadiliko yaliyotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya pamoja na maboresho yaliyokwishatekelezwa hivi karibuni na kuwa na kauli moja.
"Kama mjuavyo ugonjwa unapokwenda kwa mwanadamu haupigi hodi,hivyo muda unapokujia huna pesa za kujitibia,Bima yako itakusaidia kukuwezesha kupata matibabu sehemu yeyote hapa nchini kwetu"Alisema Kullaya.
Akifungua Mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dr Nassor Ally Hamid aliwataka Waratibu wa Mifuko hiyo
kuhakikisha dawa zinapatikana na Wahudumu wa Afya wanakuwa na Lugha Mzuri kwa wagonjwa wanaowahudumia ambapo pia aliitaka ofisi ya NHIF Pia kutumia viongozi mbalimbali wa Serikali katika kuhamasisha kutokana na Idadi ndogo ya Jamii kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii ambapo kwa mkoa wa lindi ni asilimia 6.6 tu ndio iliyojiunga na mfuko huo.
Katika kupunguza makali ya Tiba katika hospital za Binafsi licha ya
kuwa na gharama ndogo za Uchangiaji kwa kaya ambapo unalipa mara moja kupata huduma za Tiba kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Nae Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Lindi, Abdulaziz Ahmeid ameahidi kushirikiana na ofisi hiyo ili wanahabari watumie kalamu zao katika kuhakikisha Jamii inapata huduma stahiki ikiwemo kushauri pale ambapo kuna changamoto zinazochangiwa na watoa huduma sambamba na kutoa wito kwa Wanahabari kujiunga na mifuko hiyo badala ya wao kuhamasisha tu.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyoratibiwa na Ofisi ya Mkoa ya NHIF pia wito umetolewa kwa zahanati, Vituo vya Afya vilivyopo mkoani humo kutumia fursa ya kukopa Vifaa tiba kwa mikopo na nafuu Kupitia katika mfuko huo ambapo malipo yake yatakatwa kupitia madai mbalimbali wanapo wahudumia wagonjwa wa Mfuko wa NHIF