NAZIZI WA KENYA AACHANA NA MUMEWE BAADA YA MIAKA MITANO YA NDOA

Msanii wa kundi la Necessary Noise la Kenya Nazizi Hirji amethibitisha kutengana na mume wake baada ya ndoa yao kudumu kwa takribani miaka mitano.

clip_image001Nazizi, mumewe na mwanao

Nazizi alithibitisha juu ya taarifa hizo alipofanya mahojiano na Nairobi News na kuongeza kuwa hawezi kutoa taarifa zaidi lakini ni kweli ndoa yao imefikia ukingoni.

“Siwezi kutoa taarifa zaidi kuhusu hilo, lakini ninaweza kukuthibitishia kuwa ndoa imevunjika.”Alisema Nazizi.

clip_image001[6]Aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ngumu kwake kuishi Lamu yalikokuwa makazi ya familia yake na mumewe Mtanzania aitwaye Vinny, hivyo imemlazimu kurejea Nairobi ambako familia yake iliko.

“Ilikuwa ni vigumu kuishi Lamu, nilihitaji kurudi Nairobi ambako wanafamilia wangu wote wako”.

Nazizi alimalizia kwa kusema yeye na aliyekuwa mume wake ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume bado wanazungumza licha ya ndoa yao kuvunjika.

Source: Nairobi Wire, Via BONGO5

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post