Unknown Unknown Author
Title: MAWAKALA REDDS MISS TANZANIA 2014 WAANZA SEMINA LEO, HII NDIO ORODHA YAO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Napenda kuwajulisha kwamba Semina ya Mawakala wanaoandaa mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2014 inafanyika leo tarehe 25 na 26 Mac...

clip_image001Napenda kuwajulisha kwamba Semina ya Mawakala wanaoandaa mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2014 inafanyika leo tarehe 25 na 26 Machi 2014, katika ukumbi wa hotel ya Regency Park iliyopo Mikocheni jijini DSM.

Semina hii ambayo itajumuisha Mawakala zaidi ya 70 kutoka Kanda, Wilaya, Vyuo na Mikoa yote ya Tanzania itawapa nafasi Mawakala kujadili Mafanikio na Changamoto za mashindano haya ambayo kwa mwaka huu yanatimiza miaka 20 tangu yaanzishwe mwaka 1994.

Kwa mara nyingine tena Kampuni ya Swahili Media group kutoka Washington DC Marekani wamepewa kibali cha kuandaa mashindano haya kwa Watanzania wasichana wanaoishi nchini humo, ambapo mshindi wake ataungana na warembo wengine 30 watakao ingia Fainali za Taifa za mwaka huu ambazo zimepangwa kufanyika baadae mwezi wa Septemba.

Pamoja na waraka huu nawatumia orodha Kamili ya Mawakala pamoja na mikoa wanayo wakilisha.

HIDAN  RICCO.

PRO, LINO INTERNATIONAL AGENCY.

+255 715 019288

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top