Wananchi waliokussanyika Nje wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara Kuipokea Timu yao ya Ndanda Ikitokea Jijini Dar es Salaam ilipofanikiwa Kucheza Mchezo wa mwisho na Kusinda na kufanikiwa Kupanda Daraja, Hivyo Timu hiyo Kuanza Kucheza Ligi kuu Tanzania Bara Kwa Msimu wa 2014/2015.Mwandishi wa Kituo cha Radio cha Clouds Fm Ndg Shafih Dauda naye alikuwepo kushuhudia Mapokezi hayo makubwa ambayo hayajawahi kutokea Mjini Mtwara.Msafara wa magari Pikipiki Na bajaji ukiondoga maeneo ya Uwanja wa Ndege na Kuelekea Uwanja wa Mpira wa Nangwanda ambapo sherehe fupi iliandaliwa kuwalaki wachezaji pamoja na Viongozi wa Timu hiyo.
Basi lililowabeba wachezaji kutoka kampuni ya Naf Beach Hotel likiwa kwenye msururu wa Magari kuelekea uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nangwanda.Ukiachana na watu waliokuwa kwenye vyombo vya usafiri wananchi wengi walikusanyika pembezoni mwa Barabara kuwalaki wachezaji hao walipo kuwa wakipita. Hakika Hii ni Historia imeandikwa na Wachezaji hawa wa Ndanda Fc na Kupokewa kwa Maandamano makubwa ya Kihistoria Mkoani Hapa.
Kikundi cha Karate cha KIROHO SAFI wakitoa Burudani ndani ya Uwanja wa Nangwanda.Timu ya Ndanda Fc ikiingia uwanjani Tayari kwa Shughuli ya kupewa Mataji na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Katibu Tawala mkoa wa MtwaraMoja ya Bango lililokuwa Uwanjani hapo na Mashabiki wa Ndanda FcWachezaji wa Ndanda Fc wakiwa wenye furaha wakiwa wanashuhudia kinachoendelea Ndani ya Uwanja wa Nangwanda Mjini Mtwara
Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Alfred Luanda (aliyevaa suti) akiwa na Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu MTWAREFA ndugu Othman KambiMkuu wa wilaya ya Masasi ndugu Farida Mgomi naye alikuwepo ndani ya uwanja wa Nangwanda wakati wa Kuipokea Timu ya Ndanda FC
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa Miguu mtwara Ndugu Othman Kambi akiongea na wananchi waliofurika uwanja wa Umoja (Nangwanda)Mkuu wa wilaya ya Masasi akimvalisha taji la Maua Mmoja wa Viongozi wa Timu ya Ndanda FCOthman Kambi (kushoto) Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mtwara akiwa na Mratibu wa wakusaidia Timu.Katibu tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akiwahutubia wananchi waliokusanyika kuipokea Timu ya Ndanda Fc katika uwanja wa Nangwanda Mtwara.
Marino Kawishe Afisa Habari wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mtwara akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara.Shabiki akiwa Kapendeza na Jezi ya Timu ya Ndanda Fc Ndani ya Uwanja wa Nangwanda Mjini Mtwara.Shamrashamra ya mashabiki wa Ndanda Fc wakiwa katika Furaha ya Kuipokea Timu yao iliyopanda daraja na Kucheza Ligi kuu kwa msimu wa 2014/2015.
Watu walikuwa ni wengi sana kiukweli kama uonavyo ndugu msomaji hakika wakazi wa mtwara walikuwa na kiu ya kupata Timu itakayocheza Ligi kuu na mungu kaipokea dua yao Kazi ni kwao sasa kuhakikisha Timu hiyo inacheza kupitia uwanja wao wa nyumbani kwa kuukarabati ili uwe na viwango vya kucheza mechi za ligi kuu ilikuwapa raha wakazi wa Mtwara.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.