Unknown Unknown Author
Title: MAHAKAMA YATOA RUKSA KWA MAWAZIRI WAANDAMIZI WA ZAMANI, BASIL MRAMBA NA DANIEL YONA KWENDA KUTIBIWA NJE YA NCHI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi  Mawaziri Waandamizi wa zamani,  Basil Mramba...

clip_image001MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi  Mawaziri Waandamizi wa zamani,  Basil Mramba na Daniel Yona wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi baada ya kusikiliza maombi yao leo.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.

Jaji Utamwa alisema baada ya kusikiliza maombi hayo mahakama inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na ruhusa hiyo Mramba na Yona siku ya kusikiliza kesi Aprili 22, mwaka huu wahudhurie mahakamani.

Mbali na Mramba na Yona, mshtakiwa mwingine ni, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.

Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top