MAGARI YAKWAMA KWENYE BARABARA YA SOMANGA - NYAMWAGE MKOANI LINDI BAADA YA MVUA KUNYESHA

clip_image002Msululu wa mabasi ya abiria na malori yakiwa hayajui hatma ya safari yao baada ya kukwama katika kijiji cha Sinza katikati ya Somanga - Nyamwage mkoani Lindi, kutokana na barabara wanayoitumia kupatwa na uharibifu mkubwa uliotokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.Eneo hili lenye urefu wa kilometa 14,ndio eneo korofi sana kwenye barabara hii kuu itokayo Mtwara,Lindi mpaka Dar es Salaam.Katapila likifanya maarifa ya kufanikisha magari hayo kupita.Msururu bado ni mkubwa sana. Wasafiri wanaotumia magari yaliyokwama katika eneo hilo wakiwa wamesimama kuangania nini kinafanyika ili waweze endelea na safari yao.

Picha na Mdau Paul Marenga,Lindi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post