Uongozi wa Vilabu hivi viwili vikubwa hapa nchini unatakiwa kukaa chini na Mashabiki wao na kuwakanya kuhusiana na uharibifu wa Miundombinu wanaoufanya Mashabiki wao katika Uwanja huu wa Taifa,kwani kuendelea kwa vitendo hivi kunazorotesha sana soka letu.Picha zote na Othman Michuzi,Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga.
Mashabiki wa timu ya National Al Ahly wakiongea na Askari Polisi kuomba wakalizuie tatizo hilo.
Askari Polisi wakiongea na Viongozi wa Timu ya Yanga ili waweze kwenda kuwaomba mashabiki wao waaondoke katika upande ule unaodaiwa kuwa ni wa Mashabiki wa Simba. 
Mambo yalianza kama masihara huku wengine wakitaniana kabisa.
Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya wenyeji Young Africans Vs Al Ahly KIKOSI CHA NACIONAL AL AHLY
KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA LEO
1. Deogratias Munish "Dida" - 30
2. Mbuyu Twite - 6
3. Oscar Joshua - 4
4. Nadir Haroub "Cannavaro" - 23 (C)
5. Kelvin Yondani "Cotton" - 6
6. Frank Domayo "Chumvi" - 18
7. Saimon Msuva - 27
8. Haruna Niyonzima - 8
9. Emmanuel Okwi - 25
10. Mrisho Ngasa - 17
11. Hamisi Kizza - 20
Subs:
1. Juma Kaseja - 1
2. Juma Abdul - 12
3. David Luhende - 3
4. Athuman idd "Chuji" - 24
5. Hassan Dilunga - 26
6. Said Bahanuzi - 11
7. Didier Kavumbagu – 7
KICK OFF1' Young Africans 0 - 0 Al Ahly
3' Al Ahly wanalishambulia lango la Yanga lakini Dida anaokoa hatari
5' Yanga wanapata kona na inaokolewa na Al Ahly
07’ Yanga wametawala kati, Msuva na Niyonzima wanaonana vizuri. (0-0)
09’ Msuva anacheza fyongo pale. (0-0)
10’ Penaltyyyyyy hapana Refa anakataa kwa madai mshambuliaji wa Al Ahly alijidondosha. (0-0)
11’ Yanga wanapata kona ya pili inaokolewa na wachezaji wa Ahly. (0-0)
14' Yanga 0 - 0 Al Ahly
Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 Al Ahly
Dakika 20.. .
Shuti kali la umbali lililopigwa na Frank Domayo nusu litinge wavuni sharif Ahmad akaudokoa na kuutoa nje ikawa kona
Dakika 22.
okwiiiiiiiiii. . Nusura aipatie yanga goli. . Na kipa wa Al ahly anaanguka na kudai kaumia. .
Yanga 0 Al Ahly 0
DAKIKA YA 30 Mchezaji wa AL AHLY anapata kadi ya Manjano baada ya kumchezea vibaya Emanuel Okwi
DAKIKA YA 37 Yanga wanaonekana kushambulia sana Goli la AL ahly lakini wanakosa umakini na kufanya kusa nafasi nyingi za magoli ya wazi hapa
DAKIKA YA 40. .
Yanga wanashambulia kwa kasi lango la Al Ahly na kupata kona takribani 3 na kukosa magoli kupitia kwa Hamis kiiza na Emanuel Okwi. . AL AHLY wanacheza taratibu na kupoza mpira huku wakijaribu mashambulizi ya kushtukiza
DAKIKA 3 ZA NYINGEZA BAADA YA DAKIKA 45 KUMALIZIKA
Yanga Wanakosa Kona nyingine tena hapa. jumla ni Kona ya Nane hapa ndugu msomaji lakini yanga wanashindwa kuzitumia Kabisa Nafasi hizi
MPIRA NI MAPUMZIKO HIVI SASA KUTOKA UWANJA WA TAIFA
YANGA 0 – 0 AL ALHLY
KIPINDI CH PILI KIMEANZA NA HAKUNA TIMU YOYOTE ILIYOFANYA MABADILIKO KATIKA TIMU ZAO
DAKIKA 2 Yanga wanapata kona ya tisa na wanakosa umakini tena na timu ya Al alhly kuokoa hatari langoni mwao
DAKIKA YA 6 Oscar Joshua Yanga anazawadiwa kadi ya Manjano Hapa kwa kucheza rafu
Na Mabeki wa yanga wanakosa umakini hapa na kusababisha kona katika Langoni Mwao. Kona imepigwa na kuokolewa
DAKIKA YA 18: Al alhly wanaonyesha uhai hapa katika kipindi hiki cha pili kwa kuweza kupata Kona 3 katika goli la Yanga lakini nazo hazijazaa matunda.
DAKIKA YA 22 KIPINDI CHA PILI BAO NI 0 – 0
DAKIKA YA 29 KIPINDI CHA PILI
Canavaro anapata maumivu hapa baada ya kupiga mpira vibaya
DAKIKA YA 34: Yanga Wanapata nafasi nyingi za Kufunga Hapa Lakini Umakini unakuwa hafifu ndugu msomaji.
DAKIKA 36 ZAZIDI KUYOYOMA HAPA UWANJA WA TAIFA
Okwiiiiii……no ni kona hapa
Inapigwaaaaaa……Goooooooooaallllllllllll DAKIKA 37
YANGA 1 – 0 AL ALHLY
Juhudi za Emanuel Okwi na Simon Msuva na kumkuta Haroub Nadir Canavaro na kuuweka wavuni.
DAKIKA YA 40 YANGA 1 – 0 AL ALHLY
Haya ile milioni Miamoja walioahidiwa timu ya yanga na Yusuf Manji sasa Wanaelekea Kuipata Timu ya Yanga.
DAKIKA YA 44. Mabadiliko Ngasa anatoka Anaingia Said Bahanuz
DAKIKA 45 ZIMEMALIZIKA NA MPIRA UMEISHA HAPA UWANJA WA TAIFA NA YANGA KUIBUKA MSHINDI KWA USHINDI MDOGO WA GOLI MOJA
YANGA 1 – 0 AL ALHLY
Tags
SPORTS NEWS

