Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Abdalla Dadi Chikota akihutubia wananchi wa Kineng'ene kata ya Mtanda Manispaa ya Lindi
Alipokuwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya MajiBaadhi ya wananchi wa kineng'ene waliohudhuria wakimsikiliza katibu tawala mkoa wa Lindi alipokuwa akihitimisha ziara yake ya
kukagua miradi ya maji manispaa ya LindiKatibu Tawala mkoa wa Lindi Abdallah Chikota akiwa katika
ukaguzi wa miradi ya maji katika kijiji cha Ng'apa Lindi akiambata na
Viongozi wa manispaa na sekriterieti ya mkoaUjenzi wa kituo cha kutibu maji na kuyasafisha kinachojengwa
katika kijiji cha Mkupama Ng'apaBaadhi ya akina mama waliokutwa wakiteka maji katika tanki la
chanzo cha Mingoyo LindiDiwani viti maalum ambae pia ni Mwenyejiti wa kamati ya Mipango Miji manispaa ya Lindi Mhe Chingolele akionja maji ya chanzo cha maji cha Mtange mjini Lindi
Na Abdulaziz Lindi
WANANCHI wapatao 32,844 sawa na asilimia 42% kati ya 78,9841 ndio wanaonufaika na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi, Kevine
Makonda, alipokuwa akitoa taarifa ya maji na mpango wa usafi wa
mazingira (WSDP) katika ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Lindi ya
kukagua Miradi ya Maji kwa halmashauri zote za mkoa wa Lindi.
Akiwasilisha taarifa yake, Makonda alibainisha kuwa huduma ya maji
katika Manispaa hiyo siyo ya kuridhisha, kwani maji yanayozalishwa na kupatikana kwa ajili ya matumizi ni wastani wa lita 1,552,000 kwa
siku, sawa na asilimia 42% ya mahitaji yanayofikia lita 5,184,000
(5,184,000M3). kwa siku
Aidha kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Manispaa ya Lindi,ina idadi ya watu wapatao 78,841 kati yao wanaonufaika na huduma ya maji safi na salama ni 32,844 tu sawa na asilimia 42%.
Aliyataja maeneo ya Tarafa ya Lindi mjini, Mnazimmoja na
mingoyo, zikiwemo kata kumi (10) na mitaa (51), vijiji vitatu na
vitongoji (20) vinapata huduma ya maji kwa asilimia 83% kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Lindi (Luwasa).
Akimalizia taarifa hiyo ya hali ya maji Makonda alisema kuwa sera ya
Taifa ya maji (2002) inawataka watumiaji wa maji kushiriki kikamilifu
katika ujenzi, matengenezo na uendeshaji wa miradi ikiwemo kuchangia malipo ya huduma hiyo ambapo Halmashauri inaendelea kuhamasisha jamii kuunda kamati na mifuko ya maji, ambapo hadi sasa imefikia 49 yenye akiba ya ya Sh, 21,716,295/-ambazo utumika kwa matengenezo madogo madogo ya miradi midogo midogo.
Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Lindi Bw Abdallah Chikota
ameeleza kuwa hadi kufikia Decemba 2013, huduma ya maji katika mkoa ni wastani wa asilimia 39% tu, kiwango ambacho ni cha chini ikilinganishwa na kile cha kitaifa cha asilimia 57%.
Chikota amesema lengo la kitaifa ni kufikisha asilimia 67% hadi
ifikapo mwaka 2015, huku lengo la Milemia namba 7 ambalo ni la
kidunia, ambapo idadi ya watu wasiopata huduma ya maji safi na salama iwe imepungua kwa nusu sawa na asilimia 75% ifikapo mwishoni mwaka huo.
Akasema mtazamo wa kisera ya maji ya mwaka 2000, iliyopitishwa na
Serikali, ambayo ndiyo inayoongoza katika utekelezaji wake, inazingatia matumizi ya maji kuwa ni bidhaa ya kiuchumi, kijamii na mazingira, hivyo gharama za uendeshaji wake lazima zichangiwe na watumiaji husika.
Katibu tawala huyo wa mkoa wa Lindi, amesema hadi ifikapo mwaka 2020 kila mtanzania anatakiwa awe na uwezo wa kupata maji safi katika umbali usiozidi mita 400 na iwe ni haki ya kupata wastani wa lita 25 kwa kila siku.
Amesema katika kufanikisha hilo, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali
unahitajika katika kupanga uendeshaji na utoaji maamuzi kuhusu
matumizi ya maji na kutoa fursa kwa sekta binafsi utoaji huduma ya
maji na usafi wa mazingira ni jambo la lazima.
Katika ziara hiyo katika manispaa ya Lindi katibu Tawala alitembelea
vyanzo vya maji pamoja na Visima katika Vijiji vya Mingoyo, Kitumbikwela, Mtange na Kineng'ene ambapo aliagiza Uongozi wa
manispaa hiyo kuwasimamia wakandarasi ili wafanye kazi kwa Mujibu wa Mikataba ili huduma zifike kwa wakati kwa wananchi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.