Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bw Abdallah Chikota (suit nyeusi) akipewa maelezo ya Ujenzi wa Mradi wa maji katika kijiji cha Namkongo Lindi VijijiniKatibu Tawala Mkoa wa Lindi akipata maelezo mafupi ya mradi ya maji na elimu katika wilaya ya lindi janaKatibu Tawala mkoa wa Lindi Abdallah Chikota Akiongea na
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Ya Lindi alipokuwa akijitambulisha na baadae kukagua miradi miradi mbali ya halmashauri hiyo, Kushoto ni Bi Grace Mbaruku Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi
Na Abdulaziz Video,Lindi
Katibu Tawala mkoa wa Lindi, Bw Abdallah Chikota ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wila ya Lindi kuhakikisha wanakamilisha miradi ya Maji inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ili kusaidia Jamii kupata maji safi na salama bila kutumia Umbali urefu na makazi yao.
Agizo hilo amelitoa jana alipokuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya Kujitambulisha toka ateuliwe Na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo iliyokuwa wazi kufuatia kustaafu kwa Thomas Sowani aliekuwa katibu Tawala wa Mkoa huo.
Katika Ziara hiyo ambayo atakagua miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu na Maji katika Mkoa huo, Chikota alieleza kuwa Watendaji wa Halmshauri wanatakiwa kushirikisha jamii kwa maeneo wanayotekeleza mradi ili kujenga ufanisi na thamani ya kazi ambapo pia alizitaka jamii kuunda Jumuia za Maji ili kuhakikisha kila mmoja ananufaika na huduma hizo kwa gharama nafuu.
Awali akikutana na Madiwani wa Halmashauri Hiyo, Katibu Tawala huyo aliwataka Madiwani kujitoa katika kusaidia jamii zao Bila woga kwa kisingizio cha kuogopa kukosa kura katika Chaguzi kwa kusimamia ipasavyo pesa za miradi zinazoletwa katika maeneo yao ikiwemo uibuaji wa miradi ya maendeleo.
Awali katika kikao na Madiwani wa Halmashauri hiyo baadhi ya Madiwani waliahidi kutoa ushirikiano na pia walimuomba kiongozi huyo kufuatilia kwa karibu baadhi ya changamoto zilizopo katika Halmashauri hiyo ikiwemo ukosefu wa Huduma bora za Maji na ELIMU.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.