Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva Juma Kasim au unaweza kumwita Sir Nature ameweza kutoa Burudani ya aina yake kwa wakazi wa Mtwara na Vitongoji vyake walioweza kuhudhuria show yake iliyofanyika katika Ukumbi wa Kipekee wa Makonde Royal Night Club Mjini Mtwara siku ya tarehe 22/3/2014.Sir Nature aliongozana na Baadhi ya wanamuziki wenzake wa Kundi la Wanaume Halisi lenye maskani yao Mjini Dar es salaam Kule TEMEKE, wasanii hao ni DOLO, KR na JB kutoka Kundi la Mabaga Fresh.
Hizi ni Baadhi ya Picha zilizochukuliwa katika Show hiyo:Presenter na Mc Kutoka Safari Radio Fm Gozza Chuma akiwa Ndani ya Makonde Night Club akisimamia show hiyo inakwenda kama ilivyo pangwaShabiki akiji mwayamwaya na Hits zilizokuwa zikipigwa humo na Dj Ommy wa Makonde Night club kabla ya Show kuanzaDj Ommy akiwapa raha wakazi wa mtwara waliohudhuria show ya Juma Kasim Sir Nature Ndani ya Makonde Night Club Mtwara.Juma Kiroboto akiwapa burudani wakazi wa Mtwara waliofurika ndani ya Ukumbi wa Makonde Royal Night Club jumamosi ya tarehe 22/3/2014.Mashabaki wa Sir Nature wakitoa shangwe kwa kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya Ukumbi huo wa MakondeRoyal Bight Club kwa kupata show ya Nguvu kutoka kwa msanii Juma Nature
Jb Wa kundi la Mabaga fresh akiwapa burudani wakazi wa Mtwara wakati wa Show ya juma Nature ndani ya Makonde Royal Night Club MtwaraHakika ilikuwa show ya aina yake hakuna Mtu aliye keti kwani Mwanzo mwisho ni shangwe kwa wasanii wa Kundi la Wanaume Halisi wakiongozwa na Juma Nature wakitoa Burudani iliyokubaliwa na Mashabiki hao na Kufanya Ukumbi wa Makonde Royal Night Club Kuzizima.Kuanzia Kushoto ni Dolo, JB na Juma Kasini wakishambulia Jukwaa la makonde Royal Night Club siku ya Jumamosi ya Tarehe 22/3/2014 Ndani ya MtwaraMsanii wa Kundi la wanaume Halisi unaweza kumita DOLO akitoa burudani katika show hiyo ya Juma Nature ndani ya Makonde Royal Night ClubWadada hawakuwa Nyuma Kushangilia jinsi walivyokuwa wakipokea burudani kutoka kwa Kundi la Wanaume Halisi likiongozwa na Juma Nature
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.