Unknown Unknown Author
Title: JESHI LA POLISI MKOANI LINDI LAKAMATA MADAWAYA KULEVYA GRAM 58
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha Mzinga Baadhi ya madawa waliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Salum Shaban Mapande Waya zili...

RPCKamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,Kamishna msaidizi Renatha MzingaMADAWA (1)Baadhi ya madawa waliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Salum Shaban MapandeMADAWA (2)Waya zilizokamatwa kwa mtuhumiwa Abdul Mahamud ambazo
zimeyeyushwa zinasadikiwa kuwa za kampuni ya simu(TTCL)

Abdulaziz Lindi
Katika Misako inayoendelea Mkoani Lindi, Jeshi la Polisi wilaya ya
Lindi Inawashikiliwa watuhumiwa watatu kwa makosa ya kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Heroin pamoja na Miundo mbinu ya Kampuni ya simu kinyume na Sheria.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi Renatha Mzinga alieleza kuwa kwa Ushirikiano mkubwa waliopewa na wanajamii wamefanikiwa kumkamata Bw Salum Shaban Mapande(32)Mkazi wa Dar es sallam akiwa na madawa ya kulevya kete 42 kubwa na ndogo 104 zenye uzito wa Gram 58 na pesa taslim tsh 2,827,500 zinazosadikika kuwa za mauzo ya madawa hayo.WATUHUMIWAWatuhumiwa wengine waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi wa Chuo cha Utalii mjini Lindi, Masudi Mohamed(19) aliekutwa na kete 35 za bhangi huku Abdul Mahamud na Halfan Salum waliokutwa na nyaya za kampuni ya simu TTCL Zenye Uzito wa kg 5.

Akielezea matukio hayo, Kamanda Mzinga alisema kuwa Kwa sasa mkoa wa Lindi umeanza kampeni kubwa ya kupambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo kupambana kuondoa wimbi la uingizaji na uuzaji wa madawa ya kulevya ambalo kwa sasa kuna ongezeko kubwa la utumiaji na uuzaji wa madawa hayo ikiwemo pombe haramu (GONGO).

Aidha Kamanda Mzinga ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kujidhatiti na kufichua wahalifu wakiwemo wauza madawa ya kulevya ambapo Jeshi lake litatoa Ushirikiano na Usiri kwa watakaotoa taarifa zinazoashiria Uvunjifu wa Amani ikiwemo za Usalama barabarani.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top