J LO AELEZEA NAFASI YA BEN AFLECK NA DIDDY KATIKA NAFSI YAKE.

clip_image001Mwimbaji Jennifer Lopez ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa wa dunia akiwemo Diddy, Ben Affleck na baadae akaolewa na Marc Anthony.

Kwenye interview aliyofanyiwa hivi karibuni, aliulizwa kama ingetokea yuko kwenye boti baharini alafu akawaona Ben Affleck na Diddy wanaelea kwenye maji na wanahitaji msaada, huku J.Lo akiwa na nafasi ya kumuokoa mmoja tu kati ya hawa angemuokoa nani?clip_image001[6]Kwa utani J.lo alijibu akiwa anacheka na kusema angewaacha wote wafie mbele ila sekunde chache baadae akasema alikua anatania na kwamba kutoka moyoni mwake anawapenda wote na hata wao wanajua anawapenda.

Unaweza kutazama jinsi ilivyokua kwenye hii video hapa chini…

Source: millardayo.com

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post