HII NAYO KALI YA MWAKA!! NIMEPATA MUME NDOTONI.., NDOA AGOST 28 - ASEMA NISHA.

clip_image001HAYA mapya! Bidada anayefanya sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa kali ya mwaka baada ya kutangaza kupata mume ndotoni na kusambaza kadi za mwaliko wa harusi yake kupitia mitandao ya kijamii.

Stori Mix ilishuhudia kadi hiyo (cheki picha), likaona isiwe kesi, likamvutia waya ambapo alifafanua: “Ni maajabu aisee! Ni ndoto ya kushangaza sana. Yaani nimeolewa na  mwanaume mzuri sana, mweusi mrefu, ana pua ya kuchongoka. Kiukweli amenivutia sana.

“Cha kushangaza sasa, baada ya shughuli kuisha watu wakagoma kuondoka wakidai eti wamehamia hapohapo ukumbini.

Nilivyoshtuka nilichukia sana, nilitamani iwe kweli, ndiyo maana nikaamua kuweka hiyo kadi, nikialika watu waje kwenye harusi yangu Agosti 28, mwaka huu.”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post