BREAKING NEWS: MKUU WA MKOA WA MARA AFARIKI DUNIA

clip_image001MKUU wa mkoa Mara Bw John Gabriel Tuppa, amefariki dunia ghafla leo majira ya saa 4.30 asbuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Katibu tawala wa mkoa wa Mara Bw Benedict Ole Kuyan, amesema kuwa Bw. Tuppa kabla ya kifo chake leo asubuhi akiwa na afya njema alifika katika ofisi ya za mkoa na kumuaga kuwa anakwenda kufunga mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Nyamwaga wilayani Tarime.

Amesema kuwa muda mfupi baada ya kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya, alipatwa na tatizo la ugonjwa huo na muda mfupi alikimbizwa hospitali ya Tarime lakini alifariki wakati akipatiwa matibabu.

Katibu tawala huyo amesema mwili wa marehemu unasafarishwa kutoka Tarime kuja hospitali ya Musoma kwa ajili ya kuhifadhiwa wakati taratibu nyingine na maelekezo ya kiserikali yakisubiriwa kutolewa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post