Unknown Unknown Author
Title: AZAM, YANGA WAENDELEZA USHINDI, TOFAUTI YABAKIA 4
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Azam FC na Yanga wameendelea kufukuzana hii leo baada ya wote kuibuka na ushindi katika michezo yao iliyochezwa katika uwanja wa Taifa na Mk...

clip_image001Azam FC na Yanga wameendelea kufukuzana hii leo baada ya wote kuibuka na ushindi katika michezo yao iliyochezwa katika uwanja wa Taifa na Mkwakwani.

Kwa ushindi wa leo wa goli 2-0 dhidi ya Mgambo shooting imeifanya Azam FC kufikisha point 50 wakati Yanga wakifikisha pointi 46 baada ya ushindi wa goli 5-0 mbele ya Tanzania Prisons.

UWANJA WA TAIFA:
Katika dimba la Taifa kulishuhudia Yanga wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, kupitia kwa washambuliaji wake wenye kasi.

Mshambuliaji toka Uganda Emanuel Okwi alifungua kalamu ya magoli kwa Yanga baada ya kuifungia Yanga goli la kwanza katika dakika ya 20 kwa mpira wa adhabu baada ya Okwi kuangushwa nje kidogo ya eneo la Hatari.

Katika dakika ya 38 Tanzania Prisons walikosa penati baada ya Frank Hau kusukumwa na Oscar Joshua, penati iliyo pigwa na Lugano Mwangama.

Mrisho Khalfani Ngassa aliifungia Yanga goli la 2 katika dakika ya 37 akiunga krosi ya Husseni Javu aliyetokea benchi kuchukuwa nafasi ya Jerr Tegete katika dakika ya 33, na kuipeleka Azam mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Katika kipindi cha pili Hamisi Kiiza aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Emanuel Okwi aliiiandikia Yanga goli la 3 akiunga krosi ya Saimon Msuva.

Katika dakika ya 76 nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' aliiandikia Yanga goli la 4 kwa mkwaju wa penati uliotokana na kungushwa kwa Husein Javu katika eneo la hatari.

Kiiza aliitimisha kalamu ya magoli kwa Yanga kwa kuifungia goli la 5 katika dakika ya 88 na kuifanya yanga kutoka na ushindi wa goli 5-0.

UWANJA WA MKWAKWANI, TANGA
Vinara wa ligi kuu ya ya vodacom Azam FC wameendeleza wimbi lao la ushindi huku mfungaji bora wa wakati wote wa Azam FC John Raphael Bocco akiendelea kufumania nyavu za timu pinzani.clip_image002
Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Mgambo JKT, Azam FC wameibuka na ushindi wa goli 2-0.

Kwa mara ya kwanza kocha Omog aliwanzisha kwa pamoja washambuliaji John Bocco na Gaudenci Mwaikimba katika safu ya ushambuliji ambapo ilidumu kwa dakika 53, kabla ya Mwaikimba kwenda benchi na kumpisha Brian Umony katika dakika ya 53.

Dakika 10 baada ya Brian Umonyi kuingia Azam FC waliandika goli la kuongoza kupitia kwa nahodha John Bocco akiunga pasi ya Brian Umonyi.

Brian Umonyi alihitimisha ushindi wa Azam FC wa goli 2-0 katika uwanja huo wa Mkwakwani kwa kuifungia Azam FC goli la pili katika dakika 82 kwa shuti kali ambalo lilimbabatiza kipa Salehe Tendega na kuingia nyavuni.

Kwa matokeo hayo ya leo Azam FC wanaendelea kuongoza ligi kwa tofauti wa pointi 4 kwa kufikisha pointi 50 huku yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 46.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top