Ujerumani wakishangilia goli lao dhidi ya ChileRonaldo akipambana na kuweka rekodi ya mabao dhidi ya Cameroon walioizabua 5-1Messi alishindwa kuibeba Argentina dhidi ya RomaniaItalia walitepeta kwa Hispania 1-0, Diego Costa akiichezea timu yake hiyo kwa mara ya kwanzaSturridge akishangilia bao liliuloibeba England jana
UJERUMANI usiku wa jana imefanikiwa kuizabua Chile kwa kuwalaza bao 1-0, huku England nayo ikipata ushindi kama huo kwa Denmark, na Brazili ikiifanyizia Afrika Kusini kwa kuifunga kwao mabao 5-0.
Bao la Ujerumani katika mechi yake na Chile lilifungwa na Mario Gotze aliyeshirikiana vyema na Mesut Ozil. amabao Ushirikiano wa kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze na kiungo wa Arsenal Mesut Ozil ulizaa matunda jana usiku katika mchezo wa kirafiki baina ya Ujerumani dhidi ya Chile.
Wachezaji wawili walishirikiana vizuri katika goli la ushindi lilofungwa na Gotze kutoka na pasi nzuri ya mwisho ya Ozil. Mchezo ulimalizika kwa matokeo ya 1-0.Matokeo mengine ya michezo ya kirafiki ya kimataifa inayotambuliwa na FIFA iliyochezwa jana na alfajiri ya leo Hispania iliilaza Italia bao 1-0 na kudhihirisha haikuiotea kwenye Fainali za Ulaya walipoisasambua mabao 4-0 mpaka kumfanya Mario Balotelli kumwaga chozi.
Mexixo na Nigeria zenyewe zilishindwa kufungana, Ivory Coast ikitoka sare ya mabao 2-2 na Belgiaum, huku Ureno ikiifumua Cameroon kwa mabao 5-1 Cristiano Ronaldo akifunga mawili na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji wenye mabao mengi kwa timu ya taifa lake akimzidi Pauleta.
Matokeo Mengine ni kama ifuatavyo
Japan 4 - 2 New Zealand
Iran 1 - 2 Guinea
Russia 2 - 0 Armenia
Bulgaria 2 - 1 Belarus
South Africa 0 - 5 Brazil
Algeria 2 - 0 Slovenia
Namibia 1-1 Tanzania
Greece 0 - 2 Korea Republic
Hungary 1 - 2 Finland
Montenegro 1 - 0 Ghana
Czech Republic 2 - 2 Norway
Israel 1 - 3 Slovakia
Bosnia-Herzegovina 0 - 2 Egypt
Cyprus 0 - 0 Northern Ireland
Colombia 1 - 1 Tunisia
Turkey 2 - 1 Sweden
Romania 0 - 0 Argentina
Ukraine 2 - 0 United States
Austria 1 - 1 Uruguay
Switzerland 2 - 2 Croatia
Germany 1 - 0 Chile
Republic of Ireland 1 - 2 Serbia
Belgium 2 - 2 Côte d'Ivoire
Poland 0 - 1 Scotland
Wales 3 - 1 Iceland
France 2 - 0 Netherlands
England 1 - 0 Denmark
Australia 3 - 4 Ecuador
Portugal 5 - 1 Cameroon
Spain 1 - 0 Italy
Honduras 2 - 1 Venezuela
Mexico 0 - 0 Nigeria
Costa Rica 2 - 1 Paraguay
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.