Unknown Unknown Author
Title: WATU 10 WAJITOSA MAJINI WAKIHOFIA KUNASWA NA POLISI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Naibu Waziri wa Fedha akiangalia Moja ya Mtumbi unaotumiaka kuvushia Biashara za Magendo kwenye hiki kivuko haramu cha Timotheo kwenye Mto S...

clip_image001Naibu Waziri wa Fedha akiangalia Moja ya Mtumbi unaotumiaka kuvushia Biashara za Magendo kwenye hiki kivuko haramu cha Timotheo kwenye Mto Songwe.clip_image001[4]Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akifanya mahojiano na Vijana waliokutwa wakivusha sukari kutoka Malawi kuja Tanzania.Vijana hao wanadai wanalazimika kutumia njia hizi haramu kuvusha Sukari kutokana na kuwa na mitaji midogo ya biashara zao, Hivyo kupita kwenye Kivuko Rasmi cha Kasumulu wanakatwa Kodi Kubwa ambayo inawafanya wakose faida kwenye Biashara yao. (picha na Habari Mpasuko Blog)

Kyela. Zaidi ya watu 10 wamenusurika kufa maji baada ya kujitosa ndani ya Mto Songwe, wakihofia kukamatwa wakati wakivusha sukari ya magendo kutoka nchi jirani ya Malawi.

Walikuwa wanahofia kukamatwa na askari polisi waliokuwa wameongozana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, wakati alipotembelea mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu, wilayani Kyela.

Katika tukio hilo, watu hao waliamua kuitupa majini, sukari na baiskeli moja waliyokuwa wakiitumia.

Baadaye wao wenyewe walijitosa mtoni na kuanza kupiga mbizi.

Tukio hilo lilitokea juzi baada ya Naibu Waziri Nchemba na msafara wake, kuwasili katika kivuko cha Timotheo, umbali wa kilometa tatu kutoka ulipo mpaka rasmi wa Kasumulu.

Vijana hao walikuwa wanatumia mtumbwi wa jadi, kuvusha sukari hiyo kutoka Malawi na kuiingiza nchini.

Nchemba alitembelea vivuko viwili kati ya 32 ambavyo ni njia za panya zinazotumika katika kuvusha bidhaa za magendo na hivyo kulikosesha taifa mapato.

Baada ya kuvuka mto, baadhi ya vijana walitimua mbio na wengine walioshindwa kuogelea, waliokolewa na kutolewa ndani ya maji kwa tabu.

Wakizungumza baada ya kuokolewa, vijana hao walisema wanafanya biashara hiyo ya magendo kwa lengo la kupata fedha za kujikimu na kuwasomesha watoto wao.

“Tunashindwa kutumia mpaka halali kuingiza sukari hiyo nchini kwa sababu bidhaa hiyo hairuhusiwi kisheria kuingizwa nchini. Pia hatuna uwezo wa kulipa ushuru mkubwa na sisi mitaji yetu ni midogo, wengi wetu tuna mitaji ya kuanzia kilo 20 hadi 100,”alisema mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Lugano.

Alisema pia baadhi ya vijana wanaovusha sukari hiyo, hawana mitaji ya kuendeshea biashara hiyo na kwamba wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa kuingiza sukari kwa magendo na kulipwa ujira kidogo unaowawezesha kujikimu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga alisema changamoto kubwa katika kupambana na biashara ya magendo ya sukari ni uhaba wa watumishi na vitendea kazi.

Pia kukosekana kwa sukari ya Tanzania katika maeneo mengi ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Alisema wakati mwingine hushindwa kuweka mkazo wa kuzuia sukari hiyo kuingizwa nchini kutokana na hali halisi kwamba wananchi hawana sukari mbadala kwa sababu sukari ya Tanzania haipatikani kirahisi.

Kwa upande wake, Nchemba alisema amejionea ukubwa wa tatizo na kwamba Serikali italifanyia kazi ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Pia aliwataka vijana hao, kujiandaa kisaikolojia, ili kufanya biashara kwa njia halali na zinazokubalika badala ya njia hiyo inayoweza kusababisha matatizo.

Mwananchi

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top