STEVE NYERERE AFUNGUKA YAKE YA MOYONI KUHUSU LULU MICHAEL..!! NA HIKI NDICHO ALICHOSEMA.

RAIS wa Bongo Movie Unit, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemmwagia sifa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa ni binti mdogo lakini sasa anajitambua tofauti na wasanii wengine wakubwa.

lulu michealElizabeth Michael ‘Lulu’.

Akipiga stori na Ijumaa Steve alisema kuwa, mbali na umakini katika kazi zake za kisanii, sasa hivi yuko makini sana na maisha yake kiasi kwamba ni nadra sana kumkuta na skendo za kijingajinga.

clip_image002Steve Nyerere.

“Achilia mbali hao mastaa wote unaowajua wewe, mimi nikiwa kama kiongozi wa Bongo Movie siwezi kusema uongo, namkubali sana Lulu kwani ni binti mdogo na anajitambua na sasa siyo mtu wa kuendekeza mambo ya starehe kama wengine, pia huwezi kumuona viwanja kirahisi, katulia anafanya kazi,” alisema rais huyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post