Mkuu wa mkoa wa lindi,Ludovick Mwananzila akihutubia wananchi wilayani liwale kulia ni mkuu wa wilaya ya Liwale Emphreim Mmbaga
Na Abdulaziz Video,Liwale
Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila ametoa siku saba kwa wazazi na walezi wote wasio wapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa na kutakiwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu 2014.
Agizo hilo amelitoa kwa nyakati tofauti wakati anazungumza na
wananchi wa kata ya Kikulyungu, Barikiwa, na Mpigamiti alipokuwa
kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo wilaya himo.
Mwanazila alisema elimu ni suala muhimu kwa mtoto ambalo
halitakiwi kufanyiwa mchezo hivyo basi mzazi, mlezi atayekaidi agizo
hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja
na kufikishwa mahakamani.
Alisema maendeleo hayawezi kupatikana bila ya elimu hivyo basi elimu
ndiyo msingi wa kila jambo kwa kulitambua hilo ndiyo maana serikali
sikivu imeanzisha mpango wa shule za sekondari za kata nchini.
Awali mkuu wa wilaya Liwale Amphray mmbaga alisema katika wilaya yake wanafunzi 1154 wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari mwaka huu lakini hadi sasa wanafunzi 482 tu waliofika katika shule walizopangiwa .
Mmbaga alisema wanafunzi 672 hawajafika shuleni kwa sababu ambazo sio za msingi hali ambayo inatishia na kukatisha tamaa katika ustawi wa maendeleo ya elimu wilaya humo.
Wakazi wa kijiji cha Kikulyungu pamoja na maofisa wa wilaya ya
liwale pamoja na sekreterieti ya mkoa wa Lindi wakimsikiliza mkuu wa
mkoa alipokuwa akihutubia wananchi wa kikulyungu mara baada ya kukagua miradi ya maendeleoMkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila akikagua miradi ya
Maendeleo wilayani LiwaleZahanati ya Kijiji cha Kikulyungu wilayani Liwale
Nyumba ya wahudumu wa Afya kijiji cha kikyulungu
inayojengwa kwa Msaada wa Benjamin Mkapa FoundationUjenzi wa maabara shule ya sekondari Nicodemus Banduka wilyani Liwale