MAN UNITED YAAMKA, YAIPIGA CRYSTAL PALACE 2-0, VAN PERSIE AANZA, ROONEY AMALIZA NA BONGE LA BAO

clip_image001[9]Manchester United imeonyesha uhai tena baada ya kushinda mechi ya Ligi Kuu kwa mabo 2-0 dhidi ya Crystal palace.clip_image001[5]Robin van Persie ndiye alianza kufunga bao kwa mkwaju wa penalty baada ya Patrice Evra kuangushwa ndani ya 18.clip_image001Lakini Wayne Rooney ambaye ameingia mkataba mpya na Man United, akapiga bao la pili. Bao hilo lilikuwa la kuvutia, kwani aliunganisha na mkwaju ukajaa kwenye kona ya lango.

Hali hiyo inaonyesha kuinua matumaini ya mashabiki wa Man United ambao wamekuwa hawana amani kutokana na timu yao kusuasua.clip_image001[11]Kocha David ‘Daudi’ Moyes aliwaanzisha Marouane Fellaini na Adnan Januzaj ambao mara nyingi wamekuwa wakianzia benchi.

Mkongwe Rio Ferdinand pia aliongoza safu ya ulinzi ambayo imekuwa haiaminiki.clip_image001[7]Mashabiki walitupa Coin uwanjani na hapa mchezaji wayne Rooney akimuonesha muamuzi wa mezihiyo.

MATOKEO MENGINE

CHELSEA 1 Vs 0 EVERTON

MAN CITY 1 Vs 0 STOKE CITY

ARSENAL 4 Vs 1 SUNDERLAND

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post