KONGAMANO LA DINI LAMALIZIKA MKOANI MTWARA, MASWI AWA KIVUTIO KWA UWAZI WAKE KUHUSIANA NA MRADI WA GESI MTWARA

katibuKatibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini akiongea na Viongozi wa Dini toka mikoa ya Lindi na Mtwara waliohudhuria katika kongamano lilifanyika kwa siku mbili mkoani Mtwara.viongozi wa mkoaWashiriki wa kongamano hilo wakiwemo Viongozi wa Serikali wa Mikoa ya Lindi na Mtwara

Na Abdulaziz Video,Mtwara
kukamilika kwa mitambo Ya kuchakata gesi asilia iliyopo Mtwara
kutaiwezesha serikali kuzalisha umeme wa uhakika na hivyo kuondokana na gharama kubwa zinazotokana na ununuaji wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya umeme ambayo inayogharimu kiasi cha shilingi trilioni 1.6 kwa mwaka.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi katika kongamano la siku mbili kwa Viongozi wa Dini toka Mikoa ya Lindi na Mtwara mara baada ya kukagua ujenzi wa eneo la mitambo ya kusafisha gesi asilia katika eneo la Madimba mkoani Mtwara ambao utaanza mwezi wa tatu mwaka huu.

Maswi akiongea mbele ya viongozi hao pamoja na wanahabari alieleza
kuwa Wizara yake Imejipanga kuhakikisha kuwa ajira zinabaki maeneo ambayo gesi inazalishwa serikali imeamua mitambo ya kusafisha gesi asilia ijengwe katika maeneo hayo ili kuchangia maendeleo ya Mikoa hiyo.

Mitambo hiyo katika itakayoanza kujengwa katika eneo la Madimba
itakuwa na uwezo wa kusafisha gesi asilia futi za ujazo milioni 210
kwa siku na itatoka katika eneo la Mnazi Bay, Ntorya katika bahari ya
kina kirefu.

Naye mtaalamu wa masuala ya gesi kutoka Shirika la Maendeleo ya
Petroli (TPDC), Sultan Pwaga aliwaleza viongozi hao wa dini kuwa
mitambo mingine yenye uwezo wa kusafisha gesi asilia kiasi cha futi za
ujazo milioni 140 kwa siku itajengwa katika kijiji cha Songosongo mkoa
wa Lindi.

Aidha Alibainisha kuwa usimikaji wa mitambo ya kusafisha gesi katika
eneo hilo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu na majaribio ya mitambo ya hiyo yataanza mwezi Januari mwaka 2015.

Akichangia katika kongamano hilo Askofu Mkuu wa jimbo la Lindi, Bruno Ngonyani ameiomba serikali kutotumia nguvu zaidi badala yake waongeze jitihada katika utoaji wa elimu kama walivyofanya kwa Viongozi wa Dini kwa kuwezeshwa kujua maendeleo ya mradi toka uanze Kongamano la viongozi wa dini wa mikoa ya Lindi na Mtwara limefanyika tarehe 25 na 26 mkoani Mtwara na ambapo Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake za Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) zilishiriki ili kutoa elimu na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu sekta za Nishati na Madini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post