Dennis Bergkamp akipozi katika sanamu lake.
SANAMU la mwanasoka aliyeichezea klabu ya Arsenal ya jijini London miaka 11, Dennis Bergkamp limezinduliwa kwenye Uwanja wa Emirates.
Bergkamp (kulia) akiliangalia sanamu lake wakati wa uzinduzi.
Zoezi hilo lililoshuhudiwa na mamia ya mashabiki wa klabu hiyo limefanyika hapo jana kabla ya mechi ya Arsenal na Sunderland. Ambay mechi hiyo iliisha kwa Ushindi mnono wa Arsenal kuifunga Sunderland 4 – 1.
Bergkamp ambaye ni raia wa Uholanzi, alijiunga na Arsenal mwaka 1995 na kustaafu kuichezea timu hiyo ya Ligi Kuu England mwaka 2006 baada ya kuiletea mafanikio kadhaa.