Unknown Unknown Author
Title: HABARI MUHIMU:: MAWAZIRI WANNE WAFUTWA KAZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amewafuta kazi mawaziri wanne akiwemo waziri wa usafiri wa angani. Mwaka jana Stella Oduah alihusishwa ...

clip_image001Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amewafuta kazi mawaziri wanne akiwemo waziri wa usafiri wa angani.

Mwaka jana Stella Oduah alihusishwa na kashfa ya kutumia dola milioni moja unusu kununua magari mawili.

Mabadiliko haya ya serikali yanakuja mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais na wakati ambapo manasiasa kadhaa kutoka chama tawala wamehama upinzani.

Hatua ya Goodluck Jonathan kuwafuta kazi mawaziri sio jambo la kushangaza.

Hivi karibuni Rais Goodluck alifanya mageuzi makubwa ambayo yanaonekana kulenga kuboresha nafasi yake ya ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Lakini kilichowashangaza wengi ni kufutwa kazi kwa Stella Oduah.

Alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Goodluck na alikuwa mtu muhimu katika kuchangisha pesa za uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo mwaka jana Stella Oduah alihusishwa na madai ya ufisadi wakati ambapo wanigeria walikuja kujua kuwa wizara yake ilitumia zaidi ya dola milioni moja kununua magari mawili ya BMW yanayoweza kuhimili risasi.

Alikanusha kuhusika na ufisadi.

Wengine waliopoteza kazi zao ni Waziri wa maswala ya polisi, waziri wa maswala ya Niger Delta na waziri wa fedha.

Rasmi walijiuzulu lakini nchini Nigeria hii inaonekana kama sio hatua kali kwa kosa la ufisadi. Ingawa bado hajatangaza nia yake ya kuwania urais, tetesi zinaarifu kuwa huenda akawania.

Lakini huenda akakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa chama cha upinzani APC, ambao umefaidika pakubwa kutokana na wanasiasa mashuhuri kukikahama chama tawala PDP.

SOURCE:: BBC SWAHILI

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top