Unknown Unknown Author
Title: EMANUEL OKWI ATOA YA MOYONI, SOMA HAPA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo mshambuliaji mwenye kasi, Emmanuel Okwi, amesema anaumia kuona anakaa nje wakati timu yake ikipambana uwanjani. Okwi, raia wa Uganda,...

Kiungo mshambuliaji mwenye kasi, Emmanuel Okwi, amesema anaumia kuona anakaa nje wakati timu yake ikipambana uwanjani.
Okwi, raia wa Uganda, amesema ana hamu kubwa ya kuitumikia Yanga ambayo ina majukumu ya kutetea ubingwa na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.OKWI
Okwi amesema anatamani kuungana na wenzake na kupambana kwa ajili ya Yanga.

“Nasikia vibaya, naumia sana moyoni kwangu kuona nimekaa tu wakati nilitaka kucheza. Naupenda mpira, achana tu na kazi lakini ndiyo mchezo ninaoupenda.

“Nataka kucheza, nataka kuungana na wenzangu kuitumikia Yanga. Ndiyo maana nina hamu kuona mambo haya yanaisha mapema,” alisema.

Okwi ambaye usajili wake umesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (Fifa) hadi litakapopata uhakika kutoka kwa lile la kimataifa (Fifa), amekuwa akishuhudia mechi za Yanga akiwa jukwaani.

Mganda huyo aliyewahi kuichezea Simba, amekuwa akiendelea na mazoezi na hivi karibuni aliungana na wenzake kambini Bagamoyo, lakini kuhusu kucheza ataendelea kusubiri kutoka TFF ambayo inasubiri kutoka Fifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top