Arsenal wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 32 ili kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Diego Costa. mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia anamendewa kwa karibu na matajiri wa London Chelsea.Mchezaji huyo Mbrazil hadi sasa ameifungia timu yake ya Atletico Madrid jumla ya madao 19 katika msimu huu pekee katika ligi ya La Liga ya nchini Hispania.
Napoli wamesema wapo mbioni kuinasa saini ya mchezaji kiungo wa chelsea mhispania Juan Matta baada ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuweka wazi kwamba kiungo huyo ni bora akaondoka kunako Stamford Bridge. Juventus, Inter Milan, Paris St-Germain, Manchester United na Liverpool nao pia wanapigana kufa kupona kumnyakua kiungo huyo mchezeshaji mwenye kipaji cha hali ya juu japo Chelsea hawatakubali kumuuza kwa klabu yoyote ya ligi kuu England.
Mshambuliaji wa Blackpool Tom Ince, 21, ametajwa kujiunga na kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer's ili kuimarisha kikosi cha Cardiff katirisha dogo januari hii usajili ambao utawagharimu Cardiff kitita cha paundi milioni 8.
Klabu ya Chelsea inasubiria kuvuna kitita cha paundi milioni 25 kutoka Wolfsburg kutokana na mauzo ya Kevin de Bruyne. timu hiyo ya Bundesliga inamtaka mbelgiji huyo 22,wakati huo huo Atletico Madrid nao wanawania saini ya mchezaji huyo kwa mkopo.
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini anafikiria kuongeza mkataba wa Joleon Lescott, 31, mwezi huu. Beki huyo wa kimataifa wa England mkataba wake unaisha msimu huu na vilabu vingi vinamuwinda kama vile Besiktas, Tottenham, Everton, Aston Villa, Newcastle na Monaco.
Kocha Mbahili duniani lakini mwenye mafanikio makubwa uwanjani mfaransa Arsenal Wenger anapigana kufa kupona kuhakikisha anainasa saini ya mchezaji mkongwe mwenye sifa ya kufumania nyavu mshambuliaji ambaye alishawahi kukipiga na Mashetani wekundu Manchester United Dimitar Berbatov katika uhamisho wa dirisha dogo januari hii.
Chelsea wapo katika harakati za kumnasa mlinzi kisiki mswitzerland Fabian Schar anayekipiga na timu ya Basel, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ametengewa kitita kikubwa na Chelsea lakini pia anawaniwa na Arsenal na Manchester United.
Wakati huo huo Chelsea wameandaa kitita cha paundi milioni 50 ili kumnasa mshambuliaji wa Napoli Gunzalo Higuain katika uhamisho wa dirisha dogo Januari hii,japo Napoli wameshakataa kwamba hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo wa zamani ambaye aliwahi kufanya kazi na Mourinho wakiwa Madrid na kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Higuain wanasema mchezaji huyo anatamani sana kujiunga na Chelsea ili kuungana na kocha mreno ambaye ni swahiba wake mkubwa.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.