Unknown Unknown Author
Title: SASA MAMBO HADHARANI..!! DINA MARIOS NA RUBEN NDEGE "NCHA KALI" WA CLOUDS FM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani. Kwa muda m...

clip_image001SIYO siri tena! Uhusiano wa kimapenzi kati ya watangazaji nyota Bongo, Dina Marios na Ruben Ndege ‘Ncha Kali’ sasa upo hadharani.
Kwa muda mrefu Dina na Ruben wamekuwa kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakijitahidi kuuficha usijulikane na watu, lakini hata hivyo watu wa karibu hasa wanaofanya nao kazi, walifahamu juu ya uhusiano huo.

Akizungumza katika Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Radio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita kwa mara ya kwanza Dina alifunguka kuhusu kuwa na uhusiano na Ruben huku akiweka wazi kuwa ana mimba yake.

“Ni kweli baba mtarajiwa wa mtoto wangu ni Ruben Ndege ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Skylight Band. Wengi hapa kazini mnajua kuwa tulianza naye mbali. Kulikuwa na kupanda na kushuka, mara kwa mara lakini nashukuru sasa uhusiano wetu umeimarika,” alisema Dina.

Alisema, katika muda aliokuwa katika uhusiano na Ruben, kuna wakati walikuwa wakiachana na kurudiana lakini anamshukuru Mungu kwa kuwasimamia na kuwafikisha katika hatua hiyo.

Siku hiyo Dina alikuwa akiaga wasikizaji wake, kwa vile atakuwa na likizo ya uzazi ya miezi minne wakati huu akisubiri kujifungua na kumlea kichanga chake.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top