ALIYEKUWA mshindi wa Bongo Star Search (BSS) mnamo mwaka 2007 'Jumanne Iddy' (Jay Four) Amepata ajali usiku wa kuamkia leo huko Bagamoyo mkoani pwani.
Kwa mujibu wa yeye mwenyewe Jay Four akiongea kwa njia ya simu ya kiganjani leo asubuhi alisema kwamba ajali hio ilitokea mida ya saa nane usiku alipokuwa akitoka kujirusha na washkaji ambao mda mrefu hawajaonana.
Lengo ilikuwa ni kuagana nao ili leo asubuhi aanze safari ya kurudi nyumbani kwake Jijini Dar alikokita makazi yake.
Star huyo hakuishia hapo bali aliendelea kusema kwamba anamuomba mwenyezi mungu amjaalie apone haraka majeraha aliyoyapata mguuni na mkononi kwani kimya chake kwa mashabiki kimeleta minong'ono ya hapa na pale, Mbali na kuachia ngoma kadhaa mpya ikiwemo kidege ambazo hazijapata Air time ya kutosha.
Sasa akitoka Hospitali na kujiskia fresh anatarajia kuachia mzigo mwingine mkali hivyo mashabiki wake muombeeni Mwenyezi Mungu amjaalie uzima wa haraka, Kwa sasa yuko katika hospitali ya wilaya huko bagamoyo kwa matibabu zaidi.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.