Mapinduzi Cup, Kombe la Kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Usiku huu limemaliza Mechi zake za Robo Fainali na Mechi za Nusu Fainali zitashindaniwa na Timu toka Uganda dhidi ya Timu kutoka Tanzania Bara katika Mechi zote mbili.
Mabigwa Watetezi, Azam FC, wao walitinga Nusu Fainali kwa kuichapa Clove Stars, Kombaini ya Pemba, Bao 2-0, URA ya Uganda kuitungua KMKM 1-0, Tusker ya Kenya na KCC ya Uganda kutoka 0-0 katika Dakika 90 na KCC kuibuka Mshindi kwa Mikwaju ya Penati.
Simba, wakicheza Mechi ya mwisho ya Robo Fainali Uwanjani Amaan Saa mbili Usiku huu waliichapa Chuoni ya Zanzibar Bao 2-0, Bao zote zikifungwa na Ramadhan Singano.
Nusu Fainali, ambazo zitachezwa Ijuma Januari 10, Azam FC itaivaa KCC na Simba kupambana na URA.
Fainali ni Jumatatu Januari 13 kwenye Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.