HUKU Ray na Chuchu Hans wakionekana penzi lao limepamba moto, mpenzi wa zamani wa Ray, Blandina Chagula ‘Johari’ ameonekana kuwarusha roho wawili hao baada ya kutupia mtandaoni picha inayomuonesha kidoleni amevaa pete ya ndoa.
Wakizungumza na Ijumaa baadhi ya watu waliobahatika kuiona picha hiyo wamesema kuwa kitendo cha Johari kuweka picha hiyo ni sawa na kuwarusha roho wawili hao kwamba yeye atakuwa wa kwanza kuolewa kabla ya Chuchu na Ray kufunga ndoa.…
“Unajua kila mtu ana njia yake ya kufikisha ujumbe, kitendo cha hivi juzi Ray na Chuchu kujiachia bila ya kificho katika Viwanja vya Leaders Club, ambapo kulikuwa na uchaguzi wa viongozi wa Bongo Movie ni sawa na kumwambia Johari hana chake ndiyo maana na yeye ameamua kurudisha kijembe kwa staili ya kuweka picha aliyovaa pete ya ndoa ili kuonyesha kuwa yeye ataolewa ila Chuchu atachezewa tu na kutupwa,” alidai mmoja wao.
Baada ya kusikia taarifa hizo kutoka kwa wadaku hao Ijumaa lilimuendea hewani Johari ambapo alipokea simu na kusema atafutwe muda mwingine kwani alikuwa yupo bize.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.