SPURS, CHELSEA ZAONGOZA ‘KUVUNGA MAREFA!’
RAIS wa FIFA Sepp Blatter amependekeza Wachezaji wanaohadaa Marefa kwa kujiangusha makusudi ili wapate Penati au kusababisha Mpinzani aadibiwe wao ndio wapewe Kadi na kutolewa nje ya Uwanja na kukaa huko kwa Kipindi maalum ili kuzuia kushamiri mtindo huu ulioshika kasi Duniani.
Pia, Blatter ametaka Wachezaji wanaodanganya kuumia lakini hawakuumia nao wakitolewa nje kwa Matibabu wabaki huko huko nje kwa Muda maalum.
Blatter amesema: “Inakera sana kuona Wachezaji walio ‘Nusu Kufa’ wakifufuka mara tu baada ya kutolewa nje ya Uwanja!”
Aliongeza: “Refa anatakiwa kumfanya Mchezaji huyo abaki nje hadi upungufu wake uiathiri Timu yake!”
Blatter amefafanua: “Adhabu hii ya kubaki nje kwa Muda Maalum itawafanya Wachezaji wanaohadaa wafikirie mara mbili!”
Msimu huu, kwenye Ligi Kuu England, Kadi za Njano 13 zimetolewa kwa Wachezaji wanaodanganya Marefa kwa kujirusha makusudi.
Wiki iliyopita, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimponda Straika wa Liverpool Luis Suarez ambae alidai alipaswa kupewa Kadi za Njano kwa kujiangusha kwenye Mechi iliyochezwa Uwanjani Stamford Bridge ambayo Chelsea iliitwanga Liverpool Bao 2-1.
Katika Mechi hiyo, moja ya matukio ya Suarez ni pale alipokuwa akimfukuza Cesar Azpilicueta ndani ya Boksi na kugongana na Samuel Eto'o na hilo limemkera Jose Mourinho ambae alisema: “Hakuzongwa. Suarez alizidiwa maarifa na Azpilicueta ambae alikuwa na Mpira huku akitoka nje ya Boksi. Suarez akaamua kujirusha kama vile anadaivu kwenye Bwawa la Kuogelea!”
LIGI KUU ENGLAND
WACHEZAJI WENYE KADI ZA NJANO NYINGI ZA KUJIANGUSHA AGOSTI 2008 | KLABU ZINAZOONGOZA KWA KADI ZA NJANO ZA KUJIANGUSHA AGOST 2008 | ||
JINA LA MCHEZAJI | IDADI YA KADI | JINA LA CLUB | IDADI YA KADI |
Gareth Bale | 7 | Tottenham | 13 |
Fernando Torres | 3 | Chelsea | 12 |
Adnan Januzaj | 2 | Manchester United | 12 |
Liam Lawrence | 2 | Arsenal | 8 |
David Bentley | 2 | Liverpool | 8 |
Ashley Young | 2 |
|
|
Luis Suarez | 2 |
|
|
Daniel Sturridge | 2 |
|
|
Javier Hernandez | 2 |
|
|
Oscar | 2 |
|
|
Andy Carroll | 2 |
|
|
Emmanuel Eboue | 2 |
|
|
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.