Unknown Unknown Author
Title: ABIRIA WA TRENI WAANDAMANA HADI KWA MKUU WA MKOA WA DODOMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Zaidi ya Abiria 1600 kutoka Kigoma na mikoa mingineyo inayotumia Usafiri wa Treni wameandamana mpaka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma baada ya Tre...

Zaidi ya Abiria 1600 kutoka Kigoma na mikoa mingineyo inayotumia Usafiri wa Treni wameandamana mpaka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma baada ya Treni waliyokuwa wakisafiria kusimama kwa masaa kumi na moja mkoani humo kwa kile kilichodaiwa reli katika eneo la godegode mkoni Mpwapwa imeondolewa na mafuriko.clip_image002Hivi ndivyo ilivyokuwa nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa huku wasafiri hawa wakisema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa safari yao imekuwa ya Mateso tangu mwanzo ambapo wamekwama zaidi ya mara tatu na huenda sababu zilizotolewa sio za kweli.

Baada ya hali hii ya sintofahamu Dkt Rehema Nchimbi akatumia busara kama kiongozi wa mkoa na kuongea na baadhi ya abiria
Naye Stesheni Masta Mkoani hapa bwana Zakaria Kilombele amesema wamelazimika kusitisha safari ya treni hiyo kwa kuwa katika eneo na godegode na Gulwe reli imeondolewa na mafuriko na kusema TRL itahakikisha abiria hao wanapewa pesa ya chakula mpaka pale watakapoondoka.

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZILIZOCHUKULIWA STESHENI HAPOclip_image002[1]Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa kwenye foleni kuelekea kwa mkuu wa stesheni ya Dodoma, Zacharia Kilombele ambako walikuwa wanapewa pesa ya kujikimu tsh. 3500 kwa abiria zaidi ya 1500 walikwama kutokana na mafuriko.clip_image002[13]

clip_image002[11]Abiria wa treni iliyokwama Dodoma wakiwa na watoto wao wakipata chochote wakati wakisubili hatima yao,huku katika stesheni hiyo kukiwa hakutamaniki kwa uchafu unaotishia afya zao kutokana na abiria zaidi ya 1500 kutakiwa kutumia matundu manne ya vyoo.clip_image002[9]Wasafiri wa treni toka Kigoma na Mwanza kuelekea Morogoro na Dar es laam wakiwa wamelala kwenye mabehewa hawajui cha kufanya baada ya treni hiyo kushindwa kuondoka Dodoma kutokana na Maji kujaa relini Gulwe na Mzaganza.clip_image002[7]Abiria waliokuwa wakisafiri na treni kuanzia kigoma kwenda Dar es laam wakielekea kwenye ofisi ya mkuu wa stesheni ya Dodoma mara baada ya treni hiyo kukwama kuondoka kwa sababu ya mafuliko yaliyosababishwa na mvua maeneo ya Gulwe na Mzaganza.clip_image002[5]Abiria wakisongamana dirishani kupokea fedha za kujikimu 3500 zilizotolewa na shirika la reli baada train hiyo kukwama kuondoka Dodoma.clip_image002[3]

(Picha na John Banda).

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top