Unknown Unknown Author
Title: UKATILI WA KIJINSIA UNASHAMIRI LIWALE, MWANAMKE AKATWA MKONO NA MUMEWE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Abdulaziz Video Huku Dunia hivi karibuni ikiwa Imeazimisha Siku 16 za harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake huko Wilayani L...

DSC00096

Na Abdulaziz Video
Huku Dunia hivi karibuni ikiwa Imeazimisha Siku 16 za harakati dhidi
ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake huko Wilayani Liwale Mkoani
Lindi, Mkazi Mmoja wa kijiji cha Naluleo aliefahamika kwa Jina la
Shida Mapele amejeruhiwa kwa Mapanga na Mchumba wake na kumsababishia ulemavu wa kudumu baada ya kumkata mkono wa kulia na na kumjeruhi katika baadhi ya viungo,

Ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za
binadamu na uvunjaji wa haki za binadamu licha ya Mtuhumiwa
kufikishwa mbele ya Sheria Wanawake wilayani Humo wametakiwa kutetea haki zao huku wakiomba sheria Ichukue mkondo wake dhidi ya ukatili huo uliofanywa na Bw Ally Burian ambae anashikiliwa na Jeshi la Polisi

Akiongea na mtandao huu Wilayani humo, Mratibu wa Asasi ya kutetea wanawake na watoto(Liwopac)Bi Hidaya Chikawe alieleza kuwa licha ya harakati zinazofanywa na wanawake kuelimisha jamii Bado Vitendo hivyo vinashika kasi wilayani humo

Hakika kwa tukio hili ni Ishara tosha inayodhihirisha kuwepo kwa ukatili wilayani humu Hapo Awali tulizoea kusikia katika mikoa ya wenzetu lakini sasa Dunia imebadilika tunashuhudia matukio haya mara kwa mara”alieleza Chikawe

Aidha aliwataka akina mama wa liwale kuanza kujitetea kwa kufichua
uhalifu unaojitokeza kutokana na Takwimu ya mwaka jana inaonyesha
matukio hayo kuwepo kwa 2% lakini sasa hali inaongezeka kila mara
hususan kipindi hiki cha mauzo ya korosho.

Kwa Upande wao baadhi ya akinamama walisema licha ya historia ya
matukio mabaya kutokea wilayani humo tukio hili la kumsababishia
ulemavu mwanamke huyo kutokana na kukatwa kwa mapanga Walieleza walivyoguswa na tukio hilo huku wakitoa wito kwa jamii na serikali kuchukua hatua kali kwa wahusika wanaobanika na kukamatwa

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekuwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ambapo hivi karibu Mwenyekiti
wa Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi wa Polisi Bi Renatha Mzinga alianzisha kampeni ya kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na matukio hayo katika maadhimisho ya siku 16 za ukatili dhidi ya Mwanamke ambapo walifanikisha kutoa misaada na usafi katika kambi ya wazee na walemavu

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top