MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo Adam Melele ‘Swebe Santina’ amedai kuwa wasanii wakongwe wanabaniwa na watayarishaji wa filamu waigizaji wakongwe kuwashirikisha katika filamu zao kwa ajili ya uoga wa kufunikwa katika filamu zao au hata wakiambiwa na watayarishaji wengine wawatafute kushiriki katika filamu zao.
Swebe akiwa na waigizaji wenzake Chuchu Hans, na DudeSwebe Santana mwigizaji wa filamu Swahiliwood.
“ukiangalia kiukweli wasanii kama sisi wakongwe ndio tumeibeba tasnia ya filamu hadi ilipofikia hapa ispokuwa kuna tatizo moja kubwa kwa wale ambao wao wamebahatika kuwa watayarishaji, wanajua kabisa cast hii ni ya Swebe na anajua nikisimama na huyu bwana ananifunika, basi lazima akunyime kazi anaweza hata kuwaambia wengine una kazi nyingi au bei yako ni kubwa,”analonga Swebe
Swebe ni moja kati ya wasanii waliolibeba sana kundi la Kaole Sanaa Group kupitia michezo yake iliyokuwa ikirushwa katika televisheni ya ITV baadae TBC1, Swebe ameshiriki katika filamu kama Ramdhani, filamu ya Mdundiko na filamu nyingine, anaamini kuwa kila mtu ana nafasi yake kwahiyo anawaambia wasanii au watayarishaji wengine hawana sababu ya kuwa na uoga kwa kuwashirikisha wasanii wakongwe katika filamu zao
Kundi la Kaole sanaa Group ndiyo kundi lililotoa wasanii wengi wanaotamba katika tasnia ya filamu kwa sasa, baadhi ya wasaniii hao ni Kemmy, Swebe Santina, Vincent Kigosi ‘Ray’, Johari, Frank, Maya, Thea na wasanii wengine wengi wanaotamba katika tasnia ya filamu Bongo
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.