Unknown Unknown Author
Title: SSRA IMESHAURIWA KUJIKITA KATIKA SEKTA BINAFSI MKOANI MTWARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MKUU wa wilaya ya Mtwara Willman Kapenjama Ndile akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo ya siku moja ya mamlaka ...

SS3

MKUU wa wilaya ya Mtwara Willman Kapenjama Ndile akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo ya siku moja ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii kwa
viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyikaleo katika ukumbi wa Boma
mjini hapa, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya
umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari
walishiriki,

SSRAMTWAFANYAKAZI mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii SSRA wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama Ndile (Mwenyekoti na fulana ndani) MKUU wa wilaya ya Mtwara Willman Kapenjama Ndile akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo ya siku moja ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyikaleo katika ukumbi wa Boma mjini hapa, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walishiriki,

Mtwara, By Abdulaziz Video.
MAMLAKA ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA), imeshauriwa kujikita zaidi kutoa elimu katika sekta binafsi kwani kwa kiwango kikubwa bado haijafikiwa na hifadhi ya mifuko ya kijamii pia ndiyo yenye watu wengi haswa vijijini.

Ushauri huo ulitolewa Lleo na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara . Wilman Ndile, wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya hifadhi ya jamii kwa
viongozi wa Mkoa wa Mtwara yaliyofanyika katika ukumbu wa Boma mjini hapa.

“Ningeshauri mjikite zaidi katika sekta binafsi ambapo vibarua pia wanaweza kuingia katika mifuko hii ya jamii kwani wapo wengi ambao wameajiriwa ajira za muda katika makampuni ya ujenzi hapo Mkoani kwetu…. Mfano wake hawa watu wa kiwanda cha saruji cha Dangote kina vibarua wengi wanaoweza kuwa wanachama wa mifuko ya jamii” alisema Ndile na Kuongeza kuwa:

“Wenzetu nchi zilizoendelea wanajivunia kuwa na mifuko hii ya jamii ambapo kwao ina nguvu hivyo ujanja ni kuingia kwa wingi ili kuweza kunufaika katika mifuko hiyo ili kuendana na wakati wa sayansi na tekinolojia” alisema Mkuu huyo.

Aidha, katika kutoa mada kwa washiriki wa semina mkuu wa idara ya
mahusiano ya jamii kwa umma na uhamasishaji wa mamlaka hiyo. Sarah Msika, alisema kuwa wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wanatakiwa kuwa macho na maisha yao ya baadae kwani hayatabiriki hubadilika kila kukicha.

“Maisha yetu siku hizi hayatabiriki hivyo ni vizuri kujiunga katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa humo… kwani unaweza ukawa unapata fedha ya kutosha kama hutawekeza vizuri basi huwezi kujua kesho itakuwa vipi” alisema Msika.

Hata hivyo aliowanyesha washiriki wa semina faida ya kuwa katika
mifuko ya hifadhi ya jamii kwani michango huwekezwa katika vitega
uchumi mbalimbali kama majengo na akachukulia mfano wa Chuo Kikuu cha Dodoma kilijengwa na fedha za mifuko ya jamii na sasa kinanufaisha watu wengi kwa elimu inayotolewa chuoni hapo.

“Kuna faida kubwa kuingia katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii kwani fedha zake huwekezwa katika majengo na mabenki kama ilivyo Chuo Kikuu cha Dodoma kimejengwa kwa fedha hizo na sasa kinasaidia wananchi kupata elimu” alisema. Msika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top