Wafanyabiashara Kariakoo wamegoma kufungua maduka Kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za elecroniki za mamlaka ya mapato tanzania (TRA) Hii kwa sababu hawazitaki mashine za risiti walizoagizwa na TRA. Kugoma kwa wafanyabiashara hawa kumetokea siku mbili tu tangu wafanyabiashara wenzao wa mkoa wa Morogoro walipogoma kuzikataa mashine hizo.
Mitaa yote ya Kariakoo, Msimbazi, Uhuru, Lumumba, Aggrey, Mchikichi, Narung'ombe, Tandamti, Congo, kote maduka yamefungwa baada ya kutangaziwa na umoja wa wafanyabiasha.
Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine hizo
Wafanyabishara wanapinga bei kubwa ya mashine hizo
Tags
HABARI ZA KITAIFA