Muimbaji na rapper, Suma Mnazaleti amefunguka kwa kusema kuwa kuna watu wameingiza siasa kwenye muziki wa Tanzania hali inayowapoteza wasanii wenye vipaji huku wasio na vipaji wakifanya vizuri kutokana na pesa zao.
Akizungumza na Bongo5 leo Suma alisema hakuna msanii wa muziki Tanzania anayeimba kuliko Ally Kiba, ila kutokana na siasa za watu wanaotumia pesa zao kwa promo ndio wasanii wasio na vipaji wanaonekana kuwapoteza wanaoweza.
“Kuna wasanii wanajifanya wana majina makubwa hapa mjini halafu hawaimbi chochote. Tuongee ukweli kuna msanii anaimba muziki mzuri hapa Tanzania kuliko Ally Kiba? Mimi naona usiasa siasa kwenye muziki ndio ambao unawapa hizo nafasi” alisema.
“Watanzania wamepeleka kila kitu kwenye siasa,ukiangalia michezo ,muziki ,afya na elimu vyote wameviingiza kwenye siasa.Angalia swala la kufeli kwa wanafunzi mwaka jana ,Watanzania walitegemea mabadiliko makubwa kwenye elimu ,siasa imeingilia kati,wakatangaza masuala ya kufanyia uchunguzi,swala la uchunguzi likapotea kimya kimya, hatukujua matokeo ya uchunguzi wao,leo wanatutangazia kushushwa kwa madaraja ya ufaulu mpaka division 5,Watanzani tunakwenda wapi na hizi siasa siasa zetu?” alihoji
“Ufike muda Watanzania waache kurahisisha rahisisha mambo.,Taifa ni letu kwanini tusifanye mambo kwa uhakika kwa manufaa ya leo na kesho,tusipo ziba ufa leo tutajenga ukuta kesho.”
SOURCE: BONGO5.COM