MSAMA AHIMIZA KUWEKA UZALENDO MBELE TAMASHA LA KRISMASI

clip_image002MKURUGENZI wa Tamasha la Krismasi, Alex Msama amewataka wafanyakazi wake wa makampuni yake kutangaza uzalendo wa hali ya juu kwa sababu tamasha hilo nia yake ni kutangaza amani na upendo.

Akizungumza na wafanyakazi wake hivi karibuni, Msama alisema tamasha hilo litakuwa na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali sambamba na viongozi wa Tanzania.   

Msama aliyasema hayo katika maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.

“Kila mmoja mfanyakazi awe askari kwa mwenzake ili kufanikisha maendeleo ya Tamasha hilo ambalo litakuwa na dhamira ya kusaidia wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema umakini utaongezeka zaidi katika suala la tiketi ambazo zitatoka nje ya Tanzania kwa sababu ya kukwepa wizi unaofanywa na baadhi ya wasilolitakia mema tamasha hilo.

“Tunajipanga kutengeneza tiketi kutoka nje ya nchi ambazo zimepiga hatua zaidi kimaendeleo ili kukwepa wizi unaofanywa na wajanja wachache wasiolitakia mema tamasha hilo lenye lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum,” alisema Msama.

SOURCE:MICHUZI BLOG

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post