Wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wa kata ya Chinongwe na Lucheregwa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wametishia kuhama chama hicho kwa madai ya baadhi ya viongozi wa halmashauri kuingilia shughuli za ushirika nakusababisha vurugu baada ya kuwaondoa viongozi wao.
Wakizungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea katika
kata hiyo wanachama hao walisema wamefikisha kilio chao kwa uongozi wa Ccm wilaya na mkoa lakini hakuna msaada uliotolewa hadi sasa hali inayowafanya wakate tamaa na matumaini na chama hicho.
Sada Juma, alisema walichukua uamuzi wa kuomba msaada chama cha mapinduzi kwa kuwa ni chama tawala na ndicho kinachosimamia
utekelezaji wa ilani yake ikiwemo suala la kuimarisha vyama vya
ushirika.
Sada alisema chama cha ushirika Luchelegwa kimeingia kwenye mgogoro ambao unaweza kukivunja chama baada ya uongozi wa wilaya kuingia shughuli za ushirika na kuwaondoa viongozi waliokuwa wana kiongoza chama hicho.
“Tumefikisha suala hilo hadi ccm wilaya na ofisi ya mkuu wa mkoa kwani viongozi hawa wanaovuruga ushirika wanatokana na CCM lakini hakuna hatua zozote zinazo ashiria kunusuru ushirika wa Luchelegwa Usivunjike” alisema Sada
alisema kufuatia hali hiyo wakulima na wanachama wa chama hicho hawana imani na watendaji na viongozi wa halmashauri hivyo wanamuomba mkuu wa mkoa kuingilia kati mgogoro huyo ili kukinusuru chama kisivunjike.
Saidi soga alisema wakulima wanao hudumiwa na chama cha ushirika
Luchelegwa wamekata tamaa kuuza mazo yao mwenye chama hicho baada ya kutokea vurugu ndani ya chama na kulazimika kuuza mazao yao kwenye vyama vilivyoko jirani nje ya wilaya.
Soga alisema kuwa Luchelegwa Amccos ni chama kinachoongoza kwa kuwa na uzalishaji mkubwa kati ya 20 vya ushirika wilayani Ruangwa hivyo uamuzi wa kumwomba mkuu wa mkoa kuingia mgogoro huo kutokana na wanachama kukosa imani na uongozi wa halmashauri hiyo kwa lengo la kukinusuru chama na kulinda mapato ya halmashauri ya wilaya na wanachama wake.
Kwa upande mwenyekiti wa ccm wilaya Ruangwa Ali Njinjo alisema
anatambua vurugu zinazoendelea kwenye chama cha ushirika Luchelegwa lakini ofisi yake hazijapata taarifa hizo kwa maandishi.

Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.