Unknown Unknown Author
Title: AFYA: WEKA MWILI WAKO KATIKA SHAPE NZURI KWA KUFANYA MAZOEZI HAYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Skwati ni mazoezi yanayofanywa zaidi na vijana wa kisasa ili kutengeneza maumbo mazuri. Katika siku za karibuni wanawake nao wameanza kuyaje...

clip_image002Skwati ni mazoezi yanayofanywa zaidi na vijana wa kisasa ili kutengeneza maumbo mazuri. Katika siku za karibuni wanawake
nao wameanza kuyajenga maumbile kwa mazoezi hayo.

Skwati ni aina ya mazoezi ya mwili yanayosaidia kujenga na kuimarisha misuli. Aina hii ya mazoezi husaidia kujenga misuli ya miguu, mikono ya mwili mzima na tumbo.

Aina hii ya mazoezi ikifanywa kwa ustadi na umakini, inasaidia kujenga nguvu za mwili sehemu ya chini ya mwili na ya juu ambayo kitaalamu inaelezwa kuwa ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa misuli.

Mazoezi haya yanaelezwa kusaidia kuboresha ukubwa wa misuli

paleunapofanya mazoezi mengine ya mwili tofauti yakiwamo yale yanayofanywa na vifaa maalumu vya mazoezi (gym).

Skwati huufanya mwili kuwa mwepesi katika ufanyaji shughuli wa kawaida katika maisha kama kutembea, kucheza muziki, kupanda milima na nyingine nyingi zinazoushughulisha mwili na misuli.

Mtu anayefanya mazoezi ya Skwati anakuwa na nafasi nzuri ya kujenga na kuimarisha misuli  sambamba na kuiweka misuli katika
nafasi nzuri ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Inaondoa mafuta
Njia moja bora na ambayo inaleta matokeo ya haraka katika kupunguza kalori na kuchomwa kwa mafuta katika mwili ni kuimarisha misuli.

Wataalamu wa masuala ya afya na mazoezi wanasema katika kila msuli unaojengwa na kuimarishwa katika mwili, mwili hupoteza
kalori 50-70 kwa siku.

Hii ina maana kuwa kama unao uwezo wa kupunguza kiasi kikubwa cha kalori kwa siku unakuwa na uwezo vilevile wa kupunguza kiasi kikubwa cha mafuta katika mwili.

Kuimarisha viungo vya Mwili
Skwati vilvile huimarisha misuli ya miguu. Mtu anayefanya aina hii ya mazoezi huweza kuwa na miguu imara yenye uwezo wa
kutembea bila usumbufu wala kupatwa na maumivu kama ilivyo kwa watu wasio na mazoezi.

Hali hii humwezesha mtu anayefanya mazoezi haya kuwa na misuli imara inayosaidia kuleta uwiano wa uzito wa mwili na kumwezesha mhusika kuondokana na uwezekano wa kupata madhara katika mifupa.

Inazuia majeraha
Mara nyingi watu wanaovunjika viungo, kushtuka miguu au mikono ni kwa sababu wana udhaifu katika misuli na tishu zilizo katika viungo (joints).

Ufanisi katika michezo
Aina hii ya mazoezi hupendwa hupendelewa zaidi na wanamichezo hasa wale wanaoshiriki katika mbio pamoja na kuruka viunzi. Hii ni kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha misuli na kuboresha
uwezo kwa wanamichezo.
Fanya mazoezi haya kwa vipindi hadi dakika 30 kwa siku, mara tatu kwa  kwa wiki kwani ni njia ya haraka ya kuchoma mafuta mwilini.

Mazoezio ni njia ya haraka sana kwa kuchoma mafuta ya moyo na mishipa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top