YANGA FC YAPANDA HADI NAFASI YA PILI BAADA YA KUMCHAPA MTIBWA SUGAR 2-0

clip_image002La Kwanza; Wachezaji wa Yanga SC wakimpongeza Mrisho Ngassa baada ya kufunga bao la kwanza leo

Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu ya vodacom Yanga leo wamepanda mpaka nafasi ya pili kufuatia ushindi walioupata hii leo mbele ya Mtibwa sugar ya Morogoro.

Yanga leo waliwakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa TAifa na kuisurubu goli 2-0 na kupunguza tofauti ya pointi baina yake na vinara Simba SC na kufikia point 3.

Yanga walianza kupata goli katika dakika ya 5 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari aliyekuwa amefungia na TFF, Mrisho Khalfan Ngassa ikiwa ni goli lake la kwanza katika michezo miwili ya ligi kuu ya vodacom aliyocheza baada ya kumaliza adhabu yake.

Yanga ambayoleo walionyesha soka safi na kuwazidi MtibwaSugar walirejea kwenye nyavu za Mtibwa Sugar katika dakika ya 22 na safari hii alikuwa Didier Kavunbagu ndiye aliye wanyanyuwa vitini mashabiki wa yanga kwa kuifunga goli la pili.

Yanga walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0, na katika kipindi cha pili matokeo yalibakia kuwa hayo hayo japo kuwa Mtibwa sugar walijaribu kusaka goli la kufutia machozi bila kufanikiwa.

Katika uwanja wa MKwakwani, wenyeji Mgambo shooting waliendelea kuwa na hari mbaya baada ya leo kukubali kufungwa goli 1-0 na wanamagereza Tanzania Prisons ya Mbeya.

Prinsons iliwabidi wangoje mpaka dakika ya 65 kupata goli pekee la ushindi lililo fungwa na Peter Michael na kuipa Prisons point tatu muhimu na kusogea mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Ligi hiyo inataraji kuendelea oktoba 9 mwaka huu ambapo timu nane zitashuka dimbani.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post