OMBI LA SHEIKH PONDA LAKATALIWA, ARUDISHWA RUMANDE

clip_image002Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa mahakamani leo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro leo imetupilia mbali ombi la kufutiwa shitaka moja kati ya matatu yanayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Ponda anakabiliwa na mashitaka matatu; ambayo ni kutokutii amri halali, kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.

Ombi la kufutiwa shitaka moja liliwakilishwa na Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro, mahakamani hapo Septemba 17, mwaka huu, akitaka shitaka la kwanza la kutotii amri halali linalomkabili mteja wake lifutwe.

Wakili Nassoro alidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza shitaka hilo, vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo imeahiriswa mpaka Novemba 7 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza mashahidi wa kesi hiyo. Sheikh Ponda amerudiswa rumande

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post