Mgeni Ibrahimu ndiye aliye twaa taji la ushindi wa BIBI BOMBA mwaka huu iliyofanyikia Escape Two jana,Washiriki waliofika siku ya jana walikua 11 na kuchujwa hadi kubakia 5
Nao walikua ni Bi Chiku Ommary alishika namba 5 namba 4 ilishikwa na Bi Agata Mhinya na namba 3 ilishikwa na Bi Tabiza Tungalaja, namba 2 kwa Bi Vero na hatimaye namba 1 kuchukuliwa na Bi Mgeni Ibrahimu aka Bi Mgeni.
Mshindi wa taji la bibi bomba mwaka huu alizawadiwa zawadi ya kitita cha pesa za Kitanzania shilingi MILION 12 na mshidi wa pili hakutoka hivihivi nae alipata pesa za Kitanzania shilingi laki tano (500,000) na wale waliobahatika kuingia kwenye tano bora walipata shilingi laki tatu (300,000) kila mmoja.
Tags
HABARI ZA KITAIFA