HII NI SPECIAL KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED

clip_image001 
Nimeamua kukusanya Video mbalimbai za mechi tofauti za Manchester United ili kuangalia je nini kimewasibu hawa jamaa wa David Moyes Je kuna mgomo baridi kwa wachezaji kuhusu Kocha au ni vipi maana ni wachezaji wachache sana walio ongezwa kiasi kwamba wasinge weza kuharibu kombination iliyoachwa na Babu Ferg.. 
Robin Van Persie: Huyu jamaa ninoumer anapokuwa mbele ya goli anajua kufunga, lakini sasa hivi yuko wapi ndio tuseme hapelekewi mipira pale mbele kama ilivyo kuwa msimu huu? inawezekana kwani sasa mfumo ni toofauti na kocha ni tofauti pia… 
Shinji Kagawa: Waswahili wanasema Mnyonge mnyongeeni lakini Hakiyake Mpeni..Huyu jamaa fundi sana lakini Kocha Moyes Haoni umuhimu wa kuwa na mtu kama huyu katika utawala wake pale Manchester united kwani kunatetesi zinasema kuwa anataka kurudishwa Dortmund 
Wayne Rooney: Huyu jamaa ndio kwa sasa anaeibaba timu kwani ndio mchezaji pekee anaye onyesha kuhangaika kwa dhati ili kuweza kubadili matokeo pindi awapo uwanjani kufananisha na wachezaji wengine wote japo alihusishwa kutokuwa na mawasiliano Mazuri na Kocha mpya david Moyes 
Wilfred Zaha: Huyu ni mchezaji mpya Aliyekuwa wa kwanza kusajiliwa na Sir Alex meneja wa zamani wa Manchester united kabla ya msimu uliopita kuisha lakini amekuwa akikosa namba katika kikosi cha Mwalimu David moyes Japo anauwezo mkubwa na alionyesha uwezo wake katika Pre season na Katika Mechi za U21 lakini Kocha Anasema hana uzoefu wa kutosha na sasa inasadikiwa anataka kumtoa kwa Mkopo 
Adnan Januzaj: huyu kijana mdogo lakini ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa kwani ameshacheza mechi kadhaa za premier na kuonyesha uwezo wa kubadilisha mchezo lakini nae bado Kocha Moyes Hampi nafasi ya kotosha kutokana na kuwa hana uzoefu katika mechi za Premier hivi sasa Club kubwa zinamuwinda ili kupata saini yake pindi atakapo maliza mkataba na United 
Luis Nani: Winger huyu ni kati ya Mawinga bora kutokea lakini alikosa nafasi kipindi fulani wakati wa utawala wa Sir Alex pia hata sasa bado Kocha David Moyes hajaonesha nia ya dhati ya kuweza kumtumia ipasavyo…..
KIUKWELI UKIANGALIA HII MAKALA KAMA WEWE NI MPENZI WA KWELI UNAWEZA KUTOKWA NA MACHOZI KWA VICHAPO WANAVYOPIGWA HAWA JAMAA KWA SASA

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post