ANGALIA ZIARA YA MH. ZITTO INYONGA, MPANDA MAGHARIBI

clip_image001Zitto Kabwe baada ya kutawazwa kuwa Mtemi wa Ukonongo, Inyonga.Zitto Kabwe akiongea na wananchi wa jimbo la Mpanda Magharibi wakati wa ziara yake jana.Zitto Kabwe (katikati) akiwa katika pozi na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi (kulia) na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Katavi (kushoto) mara baada ya kutawazwa kuwa Mtemi wa Ukonongo eneo la Inyonga Wilaya ya Mlele mkoani Katavi

Jana nimefanya mikutano 6 katika jimbo la Mpanda Magharibi, nimepewa heshima ya utemi wa Ukonongo pale Inyonga, tumezungumza na wananchi wakulima wa tumbaku na madhila yao.

Wananchi wanadhulumiwa kwenye bei ya dola za kimarekani katika kila kilo ya tumbaku ambapo wanapewa bei ya tshs 1400 kwa dola $1 moja! Makato ya pembejeo makubwa na wanashindwa kutoka kwenye umasikini. Tukiwa Sikonge tutatoa kauli kuhusu Wakulima wa Tumbaku na namna ya kuwakomboa.

Tumezugumza umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi na namna ya kuepusha mchakato kutekwa na kundi dogo la watu wasiotaka mabadiliko. Tumezungumza kuhusu umuhimu wa mwafaka wa kitaifa katika kuandika katiba ya nchi yetu. Kuweka maslahi ya Taifa mbele ya maslahi ya vyama vya siasa.

Leo tunakwenda Mpanda Magharibi kuanzia Mpanda ndogo mpaka Ikola, Mwambao mwa Ziwa Tanganyika.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post