Mwogeleaji mwenye umri wa miaka 64 kutoka Marekani, Diana Nyad ameweka rekodi mpya ya dunia katika kuogelea baada ya kufanikiwa kuogelea kutoka Havanna Cuba mpaka huko Florida Marekani.
Ikiwa hii ni mara ya 35 mfululizo kufanya jaribio kama hili na kwa jumla ya hesabu, ameweza kukaa ndani ya bahari kwa masaa 52, dakika 54, na sekunde 18.6, na aliweza kutoka mwenyewe mpaka beach kabla ya kuishiwa nguvu kabisa.
Safari ya mwanamama huyu imekuwa na umbali wa jumla ya maili 110 sawa na kilometa 180.
Safari zote ambazo mwanamama huyu amekuwa akijaribu kuvuka bahari amekuwa akipata changamoto kama vile kushambuliwa na samaki wakali wa baharini na mambo mengi ya kufanana na hayo lakini hakukata tamaa kujaribu tena na tena na safari hii amefanikiwa bila kutumia vifaa vya kujikinga.
Mwanamama huyu amesema kuwa amejifunza kuwa katika safari kufuatilia kutimiza ndoto zako, usikate tamaa hata siku moja, na hakuna swala la kizuizi cha umri katika kufuatilia ndoto zako.
Home
»
HABARI KIMATAIFA
»
SPORTS NEWS
» MWANAMKE WA MIAKA 64 AVUNJA REKODI KWA KUOGELEA KUTOKA CUBA MPAKA FLORIDA
About Author
JE, UNA HABARI, PICHA, TANGAZO, MAKALA NA USHAURI? USISITE KUWASILIANA NASI SIMU / WHATSAPP NAMBA 0625535420.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.