Msikiti mkubwa wa barabara ya saba mjini Dodoma umewaka moto mchana huu ikiwa ni muda mfupi baada ya swala ya mchana kumalizika.
Akiongea kwa njia ya simu na Mpekuzi wetu, mmoja wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo amedai kuwa chanzo cha moto huo ni moto wa JIKO la wakazi wa ghorofa ya juu ya jengo la msikiti huo.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, moto huo umefanikiwa kudhibitiwa na jeshi la zima moto na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na moto huo.
Tunaendelea kufuatilia undani wa tukio hili.Endelea kuwa nasi
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.