Unknown Unknown Author
Title: KITUO CHA AFYA KITOMANGA NA ZAHANATI YA MILOLA MKOA WA LINDI ZAPATA GARI LA WAGONJWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Said Mtanda (mb) akihutubia wananchi katika mkutano  wa makabidiano Magari mawili ya Wagonjwa katika zahanati za Kitomanga na Milola Imeand...

SAM_0139Said Mtanda (mb) akihutubia wananchi katika mkutano  wa makabidiano Magari mawili ya Wagonjwa katika zahanati za Kitomanga na Milolaclip_image002SAM_0217

Imeandikwa na Elvan Limwagu, Lindi.

Mh. Saidi Mtanda, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mchinga Jana amekabidhi magari mawili (2) Ambulance kwa ajili ya matumizi ya Kituo cha Afya Kitomanga na Lingine katika Zahanati ya Milola. Hafla hizo zilizopambwa na Msafara wa Wana CCM zilianzia katika Kata ya Kitomanga na baadae kuhitimishwa katika Kata ya Milola.

Akizungumza kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Kazembe Hussein Mkunga alisema magari hayo ya Wagonjwa ni ukombozi kwa wakazi wa Kitomanga na Milola ambapo yatarahisisha rufaa za wagonjwa kutoka katika maeneo hayo kwenda hospitali ya Mkoa wa Lindi Sokoine.

TAARIFA FUPI YA KITUO CHA AFYA KITOMANGA KWA MHE. SAIDI MTANDA (MB) JIMBO LA MCHINGA KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA GARI LA WAGONJWA – TAREHE 09/09/2013

Mhe. Mbunge Jimbo la Mchinga;

Kituo cha Afya Kitomanga kilifunguliwa mwaka 1971. Kituo hiki kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, na kipo umbali wa km. 55 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine.

Kituo hiki kipo katika Kijiji cha Kitomanga, Kata ya Kitomanga na Tarafa ya Mipingo. Kituo hiki kinahudumia wananchi wapatao 34,909 na kutoa huduma ya rufaa kutoka Zahanati 9 (Namkongo, Mipingo, Kingurungundwa, Kilangala, Mchinga, Dimba, Mvuleni, Kilolambwani na Kijiweni). Wakati mwingine hutoa huduma ya rufaa katika Tarafa ya Nangaru na baadhi ya maeneo kutoka Wilaya ya Kilwa.

Kituo cha Afya Kitomanga kina jumla ya watumishi 14 ambao ni sawa na 48% ya mahitaji. Kada za watumishi waliopo ni kama ifuatavyo:-

i. Daktari wasaidizi - 1

ii. Wauguzi wakunga - 7

iii. Tabibu meno - 1

iv. Mteknolojia Maabara - 1

v. Wahudumu wa Afya - 2

vi. Dereva - 1

vii. Mlinzi - 1

Kituo hiki kina nyumba za watumishi (tano) 5 kati ya 13 zinazohitajika kukidhi makazi ya watumishi waliopo sasa. Kwa ujumla tuna Wadi za kulaza wagonjwa 5 kati ya hizo 3 zinatumika kwa huduma za kulaza. Pia kuna jengo la wagonjwa wa nje, X-ray, Maabara na jengo la upasuaji ambalo ujenzi wake unaendelea hivi sasa.

Huduma zitolewazo katika kituo hiki ni pamoja na:-

i. Huduma za Mama, Baba na Mtoto (uzazi).

ii. Tiba za magonjwa mchanganyiko.

iii. Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa hiari.

iv. Huduma kwa watu wanaoishi na VVU (Kutoa dawa za kupunguza makali VVU)

v. Huduma za Kinga.

vi. Kutoa rufaa kwa wagonjwa wa dharura (wajawazito) na wanaotakiwa kupata huduma katika ngazi ya hospitali.

vii. Afya ya Jamii ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ya afya kwa umma.

Mhe. Mbunge;

Kituo hiki kilipata gari la wagonjwa kwa mara ya kwanza 4/12/2003 na imekuwa ikitumika kwa zaidi ya miaka tisa mfululizo. Gari hiyo kwa sasa ni chakavu ambayo inahitaji matengenezo ya mara kwa mara hali ambayo husababisha muda mwingi kituo kukosa gari.

Kupatikana kwa gari hii kutasaidia kutoa huduma za uhakika za rufaa kwa wagonjwa mbalimbali hasa huduma ya uzazi na watoto chini ya miaka 5.

Hitimisho

Kwa niaba ya wananchi wote wa Tarafa ya Mipingo na maeneo jirani tunatoa shukrani za dhati kwa msaada mkubwa ulioutoa kwa kuleta gari hili ambalo litakuwa ukombozi katika kuboresha huduma za afya za rufaa katika vijiji vinavyozunguka kituo hiki.

Nawasilisha.

************************************************

TAARIFA FUPI YA ZAHANATI YA MILOLA KWA MHE. SAIDI MTANDA (MB) JIMBO LA MCHINGA KATIKA HAFLA YA MAKABIDHIANO YA GARI LA WAGONJWA – TAREHE 09/09/2013

Mhe. Mbunge Jimbo la Mchinga;

Zahanati ya Milola ilifunguliwa mwaka 1967, ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi km umbali wa km 56 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine.

Zahanati hii ipo katika Kijiji cha Milola A, Kata ya Milola na Tarafa ya Milola. Zahanati hii inahudumia wananchi wapatao 11,453 wa Vijiji vya Milola A, Milola B, Namtamba na Legeza mwendo.

Zahanati ya Milola ina jumla ya watumishi wataalamu wa afya 5 ambao ni sawa na 71% ya mahitaji. Kada za watumishi waliopo ni kama ifuatavyo:-

i. Afisa Tabibu - 2

ii. Wauguzi - 3

Zahanati hii haina nyumba za watumishi kabisa na hivyo kuwafanya watumishi waliopo kupanga nyumba za wenyeji mbali kidogo na Zahanati ilipo; hii ni changamoto inayohitaji kupewa kipaumbele kutatua.

Huduma zitolewazo katika kituo hiki ni pamoja na:-

i. Huduma za Mama, Baba na Mtoto (uzazi).

ii. Tiba za magonjwa mchanganyiko.

iii. Ushauri Nasaha na Upimaji wa VVU kwa hiari.

iv. Huduma kwa watu wanaoishi na VVU (Kutoa dawa za kupunguza makali VVU)

v. Huduma za Kinga.

vi. Kutoa rufaa kwa wagonjwa wa dharura (wajawazito) na wanaotakiwa kupata huduma katika ngazi ya hospitali.

vii. Afya ya Jamii ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ya afya kwa umma.

Mhe. Mbunge;

Kupatikana kwa gari hili kutasaidia kutoa huduma za uhakika za rufaa kwa wagonjwa mbalimbali hasa huduma ya uzazi na watoto chini ya miaka 5.

Hitimisho

Kwa niaba ya wananchi wote wa Tarafa ya Milola na maeneo jirani tunatoa shukrani za dhati kwa msaada huu mkubwa ulioutoa kwa kuleta gari hili ambalo litakuwa ukombozi katika kuboresha huduma za rufaa na huduma za afya katika Tarafa hii.

Nawasilisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top