BI JACQUELINE MALEKO ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE

clip_image001Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Jacqueline M. Maleko (Pichani) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo ulianza Septemba 10, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Bi. Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Masoko, Wizara ya Viwanda na Biashara, kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade.

SOURCE: AUDIFACEJACKSON BLOG

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post