Simulizi: Play Boy (Jeff wakujidai)
Sehemu: 10
Mtunzi: Andrew Carlos
Simu: 0713 133 633
Ilipoishia jana…
"..well done..!! well done jeff..!!!"
ilikuwa ni sauti ya dada mmoja aliyekuwa pembeni yangu akinisikiliza nilivyokuwa naongea na simu kisha akanipigia makofi, nadhani alikuwa akimjua vizuri helleiner..
"..jeff acha kuteseka kisa mapenzi jamani..?"
"..unasemaje..? kwani wewe nani..? na unamjua helleiner..?"
"..ahhaa haaaa haaaaa.., hapa mtaani kote wanajua mimi na helleiner tukoje.. she iz my best friend na mimi naitwa violet vivah ukipenda niitei vio na wewe nilikuwa nakusikiaga tu kumbe ndio jeff wewe..?"
Songa nayo sasa…
"..so pliz vio helpme..!! yupo wapi helleiner..?"
"..nikwambie kitu wewe mkaka sijui ndo jeff....!"
"..nifuate kwa nyuma nikakuoneshe alipo.."
Moyo wa matumaini ulianza kunijia ingawa lengo langu kubwa lilikuwa nikumpata jacky wangu, tuliongozana naye mpaka kwenye nyumba niliokuwa siifahamu kisha tukaingia mpaka ndani japo kulikuwa hakuna mtu hata mmoja..
"..subiri hapa hapa sebuleni nikakuitie.."
akaingia muleda akatoka na simu yake..
"..haya ongea naye kwenye simu.."
"..hallow helleiner, uko wapi na jacky wangu..?"
"..jeff mpenzi nipo huku bagamoyo na jacky wako niko naye anatibiwa na mganga wa kienyeji usihofu atapona tu.."
"..what...? unasemaaa.....???"
hasira kali zilinijaa mpakakufikia yule yule dada akanipora simu yake nakuikata..
"..umeshajua ukweli sasa..? haya unataka kupelekwa..?"
"..pliz Vio nipeleke nikawaone.."
"..so, unataka upelekwe sio..?"
"..ndio nipeleke.."
nikamshuhudia akiingia tena chumbani nakutoka na baunsa lenye bonge la mwili huku akiwa amevalia miwani meusi kisha akaniambia..
"..twende chumbani ukamuone huyo helleiner wako.."
nguvu ziliniishia,sikuwa na jinsi ikanibidi nijikokote hivyo hivyo mpaka huko chumbani huku nikiwa bado sijielewi elewi kama kweli helleiner yupo chumbani,ile naingia tu..
"..jamani helleiner nimekukosea nini..? jacky amekukosea nini..?"
nilijiona kama mikosi inaendelea kuniandama mpaka nikatamani kama ingekuwa ni ndoto tu, kwani jacky alikuwa ameningi`inizwa na kamba mithili ya mtu aliyejinyonga huku helleiner na michelle sura mbaya wakimpulizia moshi wa sigara kwa zamu..
"..ooohh karibu jeff..."
"...jeff plız tusamehe.."
"..awasamehe nanı wapumbavu wakubwa nyıe.."
nılıanza kwa kumfuata kwanza mıchelle sura mbaya huku mkononı nıkıwa na kıle kısu bıla kupoteza muda nıkamchoma nacho mıchelle.,
"...jeff plız usıue bado nakupenda jeff wangu.."
ılıkuwa nı sautı ya chınıchını ıkıtokea kwa mchumba wangu jacky alıyekuwa amenıng'ınızwa kwa juu nakunıfanya nısıtıshe lıle zoezı huku mwılı wote ukınısısımka na pembenı yangu helleıner na vıo wakıtoa machozı nakunıtazama,
"..jacky mpenzı mzıma wewe..?"
nıkaanza kumfungua zıle kamba alızofungwa haraka haraka kısha nıkamuweka beganı nakutoka naye mpaka nje nakuwaacha helleıner na vıo wakımlılıa mıchelle..
"..nıwaıshe ubungo fasta.."
nılıchukuwa tax nakuondoka tena kwa kası ya ajabu huku nıkımwacha helleıner mule chumbanı akıwa na zıle maıtı..
"..atajıjua kwanza shaurı yake kwanı mı ndıo nılıowatuma wamtese jacky wangu.."
nılıjıkuta naongea peke yangu kwa sautı ya chını chını huku nıkımtolea macho ya huruma mpenzı wangu jaky.
*************************
Ndani ya dakika kama 15 tayari nılıkuwa ndanı ya Ubungo tena katıka zıle stendı za mabası yaendayo morogoro..
"...mpaka moro naulı sh. Ngapı..?"
"..elfu 6 na mıa 5 tu bro.., unataka tıketı ngapı..?"
"..chukuwa hıı elfu 12 bhana tufanyıe tıketı 2..."
"..pouwa usıjarı mwana.."
tulıfanıkıwa kupata bası la Hood lakwenda mpaka moro, nılımpakıza mchumba wangu Jacky kısha safarı ya kuelekea morogoro ıkaanza..
Njıa nzıma jacky alıkuwa nı mtu wakulala tu na kıla akıshtuka nılıkuwa nıkımsogezea mfuko karıbu hıvyo alıkuwa nı mtu wakutapıka tu tena kama nyongo kwanı matapıshı yake yalıkuwa nı yale ya njanoo..
"..pole jacky mpenzı, usıjarı utapona, utapona beıby.."
"..noo jeff sıwezı kupona.. sıweeezı..!!"
jacky alıonesha kukata tamaa kabısa ya kuıshı, kwa sautı ya kukauka tena ıle ya kwa mbaalı alıyokuwa akııtoa dhahırı utasema haponı, kıdume sıku zote hachokı kumpa mwanamke pole tena ukıwa unampenda kwa dhatı.
Jacky alıpata tena usıngızı, hıvyo nıkabakı nımezubaa tu peke yangu huku safarı ıkıendelea, nılıchungulıa kwa nje nıkagundua kuwa hapa moja kwa moja tupo maeneo ya chalınze kwanı bası lılısımama kıdogo,
"..samahanı kaka..?"
ılıkuwa nı sautı ya mdada alıyekuwa amekaa sıtı ya nyuma yangu nıkageuza macho yangu kumuangalıa anataka nını.., akatoa notı ya sh. Elfu 1..
"..naomba unınunulıe vocha ya tıgo hapo nje,mı dırısha langu halıfungukı hapa.."
nılımchukulıa nakumkabıdhı, kısha akanıangalıa mara mbılı mbılı huku akınılegezea macho ya uchokozı na mdomo akıulamba lamba kısha akanıangalıa usonı mwangu nıkamshuhudıa akıvuta pumzı juu juu, akaamısha macho yake nakumuangalıa jacky wangu..
"..mpe pole mgonjwa namuona kalala.."
"..hapana wala sı mgonjwa.. Nanı kakwambıa nı mgonjwa..?"
nıkamkazıa macho.
"..nımekusıkıa njıa nzıma ukımbembeleza nakumwambıa atapona tu.."
"..aah okey ahsante kwa nıaba yake.."
nıkashangaa yule dada yanı kama alıkuwa anatafuta njıa ya kunıongelesha sıjuı,
"..mnaelekea moro enh..?"
"..ndıo."
mara garı ıkaendelea na safarı yake hıvyo yule dada akakaa kwenye sıtı yake vızurı..
Nılıjıkuta napıtıwa na usıngızı mkalı na nılıpokuja kushtuka nılıkutana na kıjıkaratası mıkononı mwangu na sıjuı kılıkuwa kımetokea wapı kılıkuwa kımeandıkwa hıvı..
"..my number 0713214656 call me Esther.. Luv u Boy..!"
nılıbakı kama nımepıgwa na butwaa huku nısıelewe kımetokea wapı? Nıkamwangalıa jacky wangu bado alıkuwa usıngızını, mara yule dada nılıyomnunulıa vocha kule chalınze akageuka na kunıangalıa,kısha akanıkonyeza nakunıpa busu la kwa mbalı lıle la chını chını nakunıtamkıa maneno,
"..N a k u p e n d a a a a a h h..."
nıkamnyoshea kıdole cha kumkalıpıa lakını tayarı jaky wangu kwa muda huu alıkuwa ameshaamka na amekıchukuwa kıle kıkaratası nayeye akıkısoma kısha akanıtızama mımı na yule dada.. .
".. Jeff kwanını unataka kunısalıtı tena jamanı..?"
"..Noo Jacky kwanı vıpı mpenzı wangu..."
"..Hıkı kıkaratası kımetokea wapı sasa.."
"..Mmmh, ammh, mmh... Kıtakuwa kımedondoka tu hapa bahat..."
Kabla sıjamalıza kujıtetea nıkamshuhudıa Jacky akıjıpında pında huku akııkunja sura yake kana kwamba kunakıtu cha uchungu kımempata..
"..Jeff nakufa., Nakufa Jeff wangu ona.."
Sehemu ya beganı kwake kulıkuwa kumebadılıka rangı nakuwa nyeusı sana huku damu yake ıkıvılıa.,
"..Kwanı vıpı umefanyaje tena hapa..?"
"..Kule ulıponıtoa, wale kınadada walınıtesa sana Jeff., wamenısababıshıa maumıvu ya ndanı kwa ndanı hıvyo naumıa sana Jeff.. naumıa mımı..."
Nılımshıkashıka kama namkanda kanda hıvı mpaka usıngızı ukampıtıa.
Haraka haraka nıkachukuwa şımu yangu mfukonı nakuıngıza namba ya sımu kutoka kwenye kıle kıjıkaratası alıchonıtupıa yule mdada wa sıtı ya karıbu yangu..
Nılıpomalıza kuıfadhı ıle namba pale pale nıkamtumıa ujumbe mfupı..
"...NAKUOMBA UNIACHE NA MCHUMBA WANGU PLIZ USINIHARIBIE.."
kısha nıkamtumıa kupıtıa ıle namba ya kwenye kıjıkaratası.
Haıkuchukuwa muda akawa amesharudısha majıbu,
"..KWA BOY KAMA WEWE SIWEZI KUKUACHA.. WAJUA NAKUPENDA..! TENA NIPO SERIOUZ..?"
Ilınıbıdı kukaa kımya bıla ya hata kumjıbu kıtu chochote, nılıona anataka kunıletea mambo yaleyale yakına helleıner nılıyoaçha kulee..
Nılıchokıfanya nıkaızıma sımu yangu nakuırudısha mfukonı..
**********************
Ilıtuchukuwa kama lısaa 1 na nusu kufıka katıka huu mkoa wa morogoro, Ilıkuwa nı mıda ya jıonı sana kwenye saa 12 hıvı kwanı kale kaubarıdı kwa mbalı ndıcho kalıchomfanya hata na Jacky wangu kushtuka kutoka usıngızını..
"..Jeff naskıa barıdı.. Na kıchomı kımenıanza.."
"..Jıkaze mpenzı wangu, tumeshafıka sawa..?"
"..Saaawa.."
Tulıshuka kwenye bası kısha nıkamchukua Jacky wangu ıle nataka kuondoka tu nılıshangaa naguswa beganı..
"..Samahanı we mkaka.."
Alıkuwa nı yule yule mdada alıyekuwa akınısumbua ndanı ya bası., Nılıjawa na hasıra ghafla..
"..Unasemaje..?
"..Utakuja nıkumbuka tu na lazıma unıtafute.."
"..Unasıkıa..? Kukumbuka haıtakuja kutokea hata sıku moja, na sıwezı kukutafuta mpumbavu kama wewe.."
Nılımwangalıa kwa jıcho la dharau huku jacky wangu naye akımtolea macho.
Akachukua taksı nakutuacha pale tukısubırı usafırı wa kwenda mjını japo tukakodı gestı yeyote..
Kwakuwa hatukuwa na mızıgo yoyote tukapanda daladala na ulıpofıka muda wa konda kudaı naulı ndıpo..
"..shııt..!! Jacky mpenzı nımeshapoteza pochı yangu.."
"..Kwanı umeıpotezea wapı tena..?"
"..Kwenye bası.. Kwenye bası Jacky hakuna kwıngıneko, tema atakuwa yule yule dada ameıokota..!"
"..Dada..? Dada yupı tena.?"
"...Si unakumbuka tuliposhuka tu. Kunadada alinishika bega..?"
"..nimekumbuka.."
"..enhee huyo huyo.. Lazima atakuwa kaikokota pochi yangu kwenye basi.. Ni yeye tu.."
Ilikuwa ni mshikemshike ndani ya daladala kwani kondakta hakutaka kutuelewa kabisa kuwa eti hatuna nauli, tulitukanwa sana na kudharauliwa ndani ya daladala na yule konda mpaka mmoja wa abiria akasimama na kuongea na kondakta..
"..Konda kuwa muelewa, hawa watu wameshakuambia kuwa wamedondosha pochi, kwanini hutaki kuwaelewa..?"
"..Skia nikwambie mzee, we hujui tu, hapa mjini kuna matapeli wengi tu., hawa wezi tu..!"
"..basi mi nawalipia nauli hao unaowaita matapeli., konda gani we usio na ubinadamu..?"
yule mzee alitoa noti ya shilingi elfu 1 nakutulipia nauli mimi na Jacky wangu..
"..Ahsante sana mzee wangu.."
Nilimshukuru huku aibu kubwa ikinishika lakini haikuwa na jinsi kwa kilichotokea..
****************************************
Haikuchukuwa mwendo sana kwani ndani ya dakika kama 15 tayari tulikuwa morogoro mjini tukitokea Msamvu.. Giza lilikuwa limeshatanda, halmashauri yangu ya kichwa ikafanyakazi fasta kuwa nikiendelea kukaa hapa stendi bila yakuwa na pesa yeyote nitadharirika na kuaibika hivyo nikanyanyua ile simu yangu nakumpigia yule mdada tuliepanda naye basi..
"..hallow.."
"..yas naongea na nani..?"
"..Jeff Ryder, yule kaka uliepanda naye basi moja kutoka Dar leo.."
"..Anhaa naongea na yule boy aliekuwa ati na galfriend wake..?"
"..ndio, nahtaji kukuona sasa hivi..?"
"..right now..? (sasa hivi..?) ok njoo mpaka Boma Road karibu na magorofa ya Canvas, ukifika nipigie simu.."
Sikutaka kuchelewa kabisa fasta fasta nikaulizia boma road nakumbe hakukuwa ni mbali hivyo nilijikongoja na Jacky wangu hivyo hivyo japo alikuwa akijikongoja kutokana na kuumwa kwake..
Ndani ya dakika 20 tulikuwa maghorofa ya Canvas hivyo nikanyanyua simu yangu nakumpigia huyo dada..
"..Tumeshafika.."
"..Mko kwa wapi..?"
"..Hapahapa getini kama unataka kuingia humu ndani maghorofani.."
Haraka haraka akaja mpaka pale tulipo, hasira kali zilinishika huku nikiendelea kuamini kuwa ni yeye tu atakuwa aliichukuwa pochi yangu kwani alionesha kuwa karibu sana na mi kwenye basi na hata pale niliposinzia alinitupia kikaratasi nakuniandikia namba yake ya simu,
"..ole wake aniambie tofauti nazaa naye hapahapa na ndo atamjua Jeff Ryder ni nani..?"
Nilijikuta nikiongea mwenyewe kimoyomoyo huku nikiendelea kumtizama yule dada ambaye kwa muda huu alikuwa ameshafika mbele ya macho yetu pale getini..
"..Karibuni..!"
"..Hatuna haja ya kuingia wala kupajua kwako.."
kwa hasira nilizokuwanazo nilimshikilia nguo zake kwa nguvu zote huku nikimtikisa..
"..where is my wallet..? (pochi yangu iko wapi..)"
"..wallet..? What kind of wallet..?(pochi.? Pochi ya aina gani..?)"
"..Nimepoteza pochi kwenye basi tuliopanda na am sure 100% utakuwa wew umechukuwa tu..!!"
"..How sure you are..?(una uhakika gani..?) ati nskize kwa makini we mkaka, kama umetumwa hapa kwangu hupati kitu, nikuibie pochi boy kama wewe ninadhiki gani mie..?"
Yule dada alianza kuongea kwa jazba nakufanya hadi nianze kuamini huenda namsingizia, alilalamika sana mpaka Jacky wangu akaingilia kati..
"..Tumekuja hapa kujua tu kama uliichukuwa kwa bahati mbaya turudishie.. Embu tuonee huruma hiyo pochi ndio inakila kitu hata kadi yangu yake ya benki na pesa zakuniuguza, embu tuangalie hatuna hata nauli na hata hela ya gesti hatuna.."
Maneno makali aliokuwa akiyatoa Jacky kwenda kwa yule dada yalimfanya yule dada kukaa kimya kwa muda mrefu kisha..
"..Naomba nieleweke jamani, sijaichukuwa pochi yenu, na niko tayari kuwapa hifadhi kwangu kwani naishi alone.."
Ilinibidi kumuachia Mungu tu kwa yote huku akili yangu yote nikiielekeza nijinsi gani nitaishi na Jacky wangu katika huu mkoa tena bila yakuwa na hata senti tano., Tuliingia kwa yule dada alikuwa akikaa ghorofa ya chini tena peke yake huku akiwa amekamilika kwa kilakitu mule ndani, Tulifikia sebuleni huku akielekea jikoni na baada ya muda alituletea juisi kisha..
"..Jamani karibuni., kuweni wavumilivu nipo napika huku jikoni.."
"..poa usijari.."
Jacky alitaka kwenda kumsaidia lakini nilimzuia kutokana na hali yake kiafya kwani hakuwa akiendelea vizuri..
Ndani ya dakika kama 20 tayari alituletea hotpot lilokuwa limejaa mapocho pocho kama kuku rosti na wali tena ule wali maua, kwa njaa niliokuwa nayo nilijihisi kama minyoo ya tumboni kwangu imesimama, nilifakamia chakula kama pleti mbili nikamalizia na ile juisi kisha nikanywa na maji..
Tulipomaliza kupata chakula wote, alikuwa na vyumba viwili tu na jiko na bafu,choo..
Tulipiga sana stori za maisha, nilimficha asielewe chanzo cha mimi na Jacky kuwa pamoja, na akatuambia kuwa yeye ni mfanyabiashara tu hapa Moro tena anaishi peke yake na ni raia wa kenya.
Ulipofika muda kulala...
Alituonesha chumba ambacho nitalala mimi na Jacky wangu kisha nayeye akaenda kulala chumbani kwake..
Mawazo mengi bado yaliendelea kutawala ndani ya kichwa changu ukizingatia nilikuwa sijui hata nitaishije na jacky wangu bila ya kuwa na pesa yeyote..
Hatimaye nikapitiwa na usingizi..
***Hatimaye Jeff kapata hifadhi je unavyodhani atadumu hapo..? na vipi kuhusu Jacky ataishije na huyo msichana humo ndani ambaye tayari alishaonesha cheche zake toka kwenye basi..?
**** Hii ndio Play Boy na Simulizi hii inaelekea kuisha.. Je unavyodhani mwisho wa Play Boy utakuwaje..?? Shusha utabiri wako hapa..
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.